January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makalla ampongeza Lissu kukiri CHADEMA haina wagombea Serikali za Mitaa

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) CPA Amoss Makala amesema Chama hicho Kipo tayari na kimethibitisha kushika dola lakini CHADEMA haina uwezo huo na Makamu Mwenyekiti wao Tundu Lissu amekiri hadharani.

Akizungumza na wanachama wa CCM Jijini Dar es Salaam ,CPA Makalla amesema jana Tundu Lissu ameeleza wazi wao hawawezi kwa hali iliyopo kusimamisha wagombea kila sehemu na anampongeza Lissu kwa kuwa mkweli kuliko Mwenyekiti wake  Freeman Mbowe aliyeitisha kikao cha makamanda wote wa Dar wa Salaam kwamba atakayeshindwa kusimamisha Mgombea katika kijiji,kitongoji au mtaa watamfukuza.

“Nataka uwafukuze  kwasababu Tundu Lissu amekiri haiwezekani na hamjasimamisha wagombea ,tafsiri yake ni nini? CHADEMA hawako tayari kushika dola, kwanza dola haishikwi kwa kuweka wagombea wachache CCM ndio iko tayari imethibitisha kwa vitendo kwa kuweka wagombea kila sehemu,tuko tayari kushika dola.

“Tundu Lissu amesema amefanya tathimini idadi ya wagombea wanaopaswa wao kuwaweka sio chini ya 380,000 na hivyo kwao hataweza kwani hiyo itakuwa ni miujiza.”amesema.