Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Mwenezi wa chama cha Mapinduzi CCM Taifa Amos Makala ,amewataka wana ccm wilaya ya Ilala wasibwete katika uchaguzi wa Serikali za mitaa badala yake wafanye kampeni kuakikisha ccm inashika dola na kushinda mitaa yake yote 159.
Amos Makala alisema hayo katika ziara yake wilayani Ilala ,kuongea na wagombea wa Serikali za mitaa pamoja na viongozi wa chama hicho mara baada kura za maoni kumalizika.
“Nawaomba wana ccm wilaya ya Ilala muwe wamoja umoja ni ushindi mkoa Dar es Salaam Chama cha Mapinduzi CCM kiko imara mkoa una mitaa 564 muwe wa moja mtashinda na Ilala ina mitaa 159 yote itarudi ccm nawaomba wanachama wa cha Mapinduzi CCM msibweteke kampeni ziendelee kama kawaida ccm ipo imara itakikisha inashika dola ” alisema Makala.
Makala aliwapongeza wote walioshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa Mwaka 2024 katika kura za maoni ccm imeonyesha ndio chama pendwa Tanzania na baada kura za maoni ndio chama pekee imesimamisha wagombea kila kitongoji.
Aliziomba kamati za siasa za kata,matawi,na kamati za kampeni kuakikisha ccm ina shika dola mkoa Dar es Salaam imejiandikisha kwa kishindo hivyo wote wapige kura .
Alitumia fursa hiyo kuwapongeza Mabalozi wa shina ,Mabalozi wamefanya kazi nzuri ,Mabalozi wanakaa na wanachama, Mabalozi wanakaa na wapiga kura wamefanya kazi nzuri kwa maslahi ya chama chao.
Alisema ccm itafanya kampeni zake za kistarabu kuakikisha Wenyeviti wake wanashinda waweze kushika dola ,kuisaidia Serikali utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi.
Alisema Wenyeviti wa Serikali za mitaa wana jukumu kubwa sana katika kujenga mahusiano mazuri na viongozi wa chama na Serikali katika kuleta maendeleo uwezi kujenga kituo cha afya au shule lazima umshirikishe Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa eneo husika.
Aliwataka Wenyeviti wa Serikali za mitaa waliokosa nafasi mwaka huu kura azikutosha au hawakuteuliwa badala yake wavute subira wagombee Udiwani mwaka 2025 katika uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani..
Wakati huohuo, Amos Makala aliwataka wagombea Wenyeviti walioteuliwa washirikiane pamoja na wagombea waliokosa uteuzi ili kuakikisha ccm inashika dola .
More Stories
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua
Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa
Vikundi Ileje vyakabidhiwa mikopo ya asilimia 10, DC Mgomi avipa somo