Na Penina Malundo, Timesmajira Online
WAFANYAKAZI kwa Kampuni ya Kivuli Bussiness Care (KBC), wazalishaji wa gazeti la Majira na Mitandao ya Kijamii imewafuturisha wafanyakazi wake katika kuadhimisha kumi la mwisho ya mwezi Mtukufu wa ramadhani.
Hafla hiyo ilifanyika leo Aprili 7,2024 jijini Dar es Salaam, katika Ofisi za Kampuni hiyo, ikiwakutanisha wafanyakazi wake kutoka maeneo mbalimbali.
Akizungumza mara baada ya Iftari hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni ya KBC, Imma Mbuguni aliwashukuru wafanyakazi hao kwa kuhudhuria hafla hiyo ikiwa ni moja ya ushirikiano baina ya wafanyakazi na kampuni hiyo.
Amesema, mwezi huu mtukufu ni mwezi wa kukaa pamoja na kula pamoja katika kumuomba Mungu kubariki kwa kila lililo jema.
”Leo tumejumuika pamoja na Wafanyakazi wa Kivuli katika Iftari ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, ikiwa na lengo la kuwakutanisha wafanyakazi wote kwa pamoja,”amesema na kuongeza
”Huu ni mwanzo mzuri wa kampuni yetu katika kujenga mahusiano mema kuhakikisha tunatoka hapa tulipo na kusonga mbele kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu,”amesema.
Akizungumzia hafla hiyo, Meneja wa Masoko wa Kampuni hiyo, Vivian Msilu kwa niaba ya wafanyakazi hao amemshukuru Mkurugenzi huyo kwa kuwakumbuka wafanyakazi katika Iftari na kumuombea Mwenyezi Mungu kumzidishia baraka.
”Tunashukuru sana kwa hatua hii, ni jambo jema mlilolifanya katika kujenga mahusiano na wafanyakazi hususan kipindi hiki cha mwezi wa ramadhani,”amesema.
More Stories
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais