Na Angela Mazula, TimesMajira Online
KINARA wa magoli ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), Prince Dube ameshindwa kujiunga na timu yake ya Taifa ya Zimbabwe baada ya kupata majeraha katika mchezo wao uliopita dhidi ya Kagera Sugar.
Katika mchezo huo uliochezwa Oktoba 4, Azam ilipata ushindi mnono wa goli 4-0 Prince akifunga goli mbili na kufikisha goli tano zilizomuweka kileleni mwa orodha ya wafungaji bora msimu huu.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ amesema kuwa, tayari wameshawataarifu timu ya Taifa ya Zimbabwe kupitia ripoti ya iliyotolewa na daktari wa timu hiyo.
“Tayari tumeshawataarifu Chama cha soka cha Zimbabwe kupitia ripoti ya daktari kuwa Prince hatojiunga na timu ya Taifa inayojiandaa na mchezo dhidi ya Malawi utakaochezwa Oktoba 11, ” amesema Zaka.
Kuhusu mshambuliaji Obrey Chirwa, Zaka amesema kuwa, hatokwenda tena kujiunga na wenzake katika kikosi cha timu ya Taifa ya Zambia baada ya kuchelewa ndege.
Baada ya mchezo wao dhidi ya Kagera, Chirwa alitakiwa kuondoka alfajiri ya Oktoba 5 na baada ya kuchelewa ilitumwa tiketi nyingine ya ndege ambayo ilimtaka kuondoka juzi Oktoba 6 saa 2 usiku lakini baada ya kuwasiliana na Meneja wa timu ya Taifa alipofika uwanja wa ndege, alimwambia kocha ameghairi hivyo atatoa tarehe nyingine.
Lakini licha ya Ligi kusimama kwa siku kadhaa kupisha maandalizi ya mchezo wa Kimataifa wa kirafiki utakaochezwa Oktoba 11 kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Burundi, kikosi cha Azam kitaendelea na maandaliai ya mchezo wao ujao utakaochezwa Oktoba 15 dhidi ya Mwadui.
Tayari kikosi chao kineanza mazoezi jana jioni na yataendelea hasi siku ya mchezo kwani mipango yao ni kuchukua alama tatu katika kila mchezo ili kujiweka kwenyw nafasi nzuri ya kutimiza mikakati yao.
Wachezaji wanaokosekana katika maandalizi hayo ni wale walioitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ambao ni David Kisu, Abdallah Sebo, Iddy Nado na Salum Abubakar pamoja na Yacub Mohammed aliyejiunga na timu ya Taifa ya Ghana pamoja na Nico Wadada wa Uganda.
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM