Na Mwandishi wetu, Timesmajira
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezindua kituo kipya cha Mabasi cha Nzega mjini ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 4.327.
Akizungumza baada ya kuzindua kituo hicho leo Machi 13,2025 ambacho utekelezaji wake umefikia asilimia 100, Majaliwa ameipongeza halmashauri hiyo kwa uamuzi wa ujenzi wa kituo hicho kwani kitaibua fursa za biashara kwa wakazi wa eneo hilo.
“Kituo hiki ni kizuri na kimejengwa kwa ubora, kituo hiki kinatakiwa kianze kutumika ili wananchi waanze kunufaika nacho, Watumishi wa halmashauri ongozeni Wana-Nzega kunufaika na fursa katika eneo lenu”
Aidha, Majaliwa ametoa wito kwa halmashauri hiyo kuongeza vibanda vya wafanyabiashara badala ya vichache ambavyo vimejengwa mpaka sasa.

“Tunataka wananchi wengi zaidi wanufaike, ongezeni vibanda, huu ni ubunifu mzuri sana utasababisha wengi wanufaike, waleteni wajasiriamali hapa wapate rizki zao, mkifanya hivyo mtaongeza mzunguko wa fedha”
Kadhalika, Majaliwa amesema kuwa Serikali inaendelea na mpango kazi wake wa kuwahudumia watanzania wakati wote, “Serikali hii ya Chama cha Mapinduzi inaendelea kukamilisha malengo yake katika kuwatumikia watanzania ninajua hatua tuliyoifikia”.
Katika hatua nyingine, Majaliwa ametoa wito kwa watumishi wa halmashauri nchini kuendelea kujielekeza katika kutatua changamoto za wananchi
“Tumueni mapato yenu ya ndani kutekeleza miradi
More Stories
JKT laonya wanaoghushi vyeti vya Mafunzo JKT
SEforALL kuimarisha ushirikiano upatikanaji nishati endelevu
Kwaya ya FFC yatoa msaada wa mahitaji mahabusu ya watoto Upanga