Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasilisha salaam za pole kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kwamba anafuatilia hali ya Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kwa ukaribu na anamuombea afya njema.
Salamu hizo amezitoa leo jijini Johannesburg, Afrika Kusini wakati akimwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa anayeendelea na matibabu Afrika ya Kusini.
“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anafuatilia hali ya Mheshimiwa Lowassa kwa ukaribu na anamuombea afya njema.”
Kwa upande wake, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Regina Lowassa amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa jinsi ambavyo amekuwa karibu na wanafamilia na namna ambavyo anafuatilia matibabu ya mpendwa wao.
Naye mtoto mkubwa wa Lowassa na Mbunge wa Monduli, Bw. Fredrick Lowassa amewashukuru Watanzania kwa maombi yao ya kumtakia afya njema baba yao.
More Stories
Simbachawene:Waombaji wa ajira jiungeni na Mfumo wa Ajira Portal
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki