November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Maisha Fiti kukuza ustawi wa mwili na akili

Na Penina Malundo, timesmajira

KAMPUNI ya Bima ya Afya ya Jubilee imezindua rasmi mpango wake wa Ustawi wa Maisha Fiti kwa lengo la kukuza Ustawi wa kimwili na kiakili kwa wateja wake.

Ameyasema hayo Novemba 10,2023 ,
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Afya ya Jubilee, Dkt. Harold Adamson wakati wa uzinduzi wa Mpango huo,amesema Maisha Fiti itawawezesha wateja kuchukua udhibiti wa Afya zao za Kinga na tiba.

Amesema mpango huo utaunda Jumuiya kwa watumiaji kuwasiliana na wenzao pamoja na wataalam wa matibabu kuhusu masuala mbalimbali ya mada kama vile Lishe,usimamizi wa maisha ,Afya ya uzazi na akili .

Amesema katika miaka ya hivi karibuni,jamii ineshuhudia kuongezeka kwa magonjwa na Hali ambazo zinaweza kuhusushwa moja kwa moja na mtindo wa maisha.

“Shirika la Afya Duniani linaripoti kuwa watu Milioni 41 hupoteza maisha Kila mwaka duniani kutokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza,”amesema na kuongeza

“Kufanya wa mazoezi unakuza ustawi wa kimwili na kiakili kwa wananchi ili kukabaliana na ongezeko la maambukizi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza,”amesema.

Amesema Tanzania kama nchi nyingi za kipato cha chini na kati inakabiliwa na mzigo mkubwa wa magonjwa ambapo takwimu za hivi majuzi kutoka Wizara ya Afya zilionesha kuwa maambukizi ya magonjwa hayo kama shinikizo la Afya zilionesha kuwa asilimia 25.9,kisukari asilimia 9.1 yamefikia viwango vya kutisha.

“Magonjwa yanayohusiana na mtindo wa maisha sio tu huathiri ubora wa maisha ya mtu binafsi lakini pia huweka mzigo mkubwa kwa rasilimali za familia na taifa. Shughuli za kimwili, unywaji pombe kupita kiasi na lishe duni zimetambuliwa kwa sababu kuu za kuongezeka kwa mzigo wa magonjwa,”amesema Dkt.Adamson.

Wakati huo huo Kampuni hiyo imezindua kampeni iliyopewa jina”fanya lolote kwa hatua ” ili kuwahamasisha watu kujumuisha mazoezi ya mwili katika maisha yao ya kila siku.

“Kampeni hii itawahimiza watu kufanya shughuli kama vile kutembea, kukumbia au kuendesha baskeli ili kuongeza viwango vya nishati na uchangamfu kwa ujumla kufanya maisha yawe ya kufurahisha zaidi,”amesema Dkt.Adamson.

Kwa upande wake Mwakilishi wa TIRA meneja Kanda ya Mashariki, Bahati Ogolwa amesema maisha fiti App imezinduliwa mahsusi kwaajili ya kupata taarifa ya Afya kwa umma,kubadili mtindo wa maisha kulinda Afya na kurahisisha ubadilishaji wa taarifa huduma.

Amesema tayari bunge limepitisha mswaada wa afya kwa wote hivyo Maisha Fiti App itasaidia kuwa sehemu ya sheria hiyo itakapoanza kutumika.

“Maisha Fiti App itasaidia matumizi ya tehama na ubunifu kwa maendeleo ya uchumi wa Taifa,muhimu kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan katika kuweka juhudi ya kuimarisha na kuendeleza sekta ya tehama nchini pamoja na kuanzisha digital Economic 2023 chini ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,”amesema.