Na Mwandishi wetu Timesmajira Online, Mbeya
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya,Mhandisi Maryprisca Mahundi,amewataka wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini kusoma kwa bidii badala ya kuendekeza anasa wawapo vyuoni.
Mahundi ameyasema hayo katika madhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mbeya(CUoM).
Profesa Ernest Kitindi,amesema ujumbe uliotolewa na Naibu Waziri huo umekuja kwa wakati na wanachuo wakizingatia watafika mbali zaidi.
Profesa Aulelia Temba amesema historia ya maadhimisho hayo yaliasisiwa nchini Marekani na yameleta mabadiliko kwa wanawake duniani,
Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho, Profesa Romuald Haule,amesema awali wanawake wamefanya matendo ya huruma katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya kwa kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo runinga (television) tano,vifaa vya usafi,pampas na taulo za kike,
More Stories
MSIGWA:Mfumo wa usajili waandishi wa habari kidijitali upo mbioni kukamilika
Kongani ya Viwanda ya Sino _Tan kutoa ajira laki moja
Waandishi wa habari kutambulika kidijitali