Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
NAIBU waziri wa habari Teknolojia ya mawasiliano na habari ambaye pia ni Mbunge wa vitimaalum mkoa Mbeya,Mhandisi Maryprisca Mahundi amekabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa waathirika wa maporomoko ya mlima Kawetele kata ya Itezi Jijini hapa.
Msaada huo umekabidhiwa leo April 17,2024 Baraka Mlonga ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation(MWEF)amesema Mkurugenzi wake Mhandisi Maryprisca Mahundi alitamani kuwepo lakini yupo nje ya nchi hivyo wapokee msaada huo na uwe faraja kwa waathirika.
“Mkurugenzi wetu ambaye ni Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Mbeya alipenda kuwepo kuwafariji ndugu zetu hawa waliopatwa na maafa ,ila sisi tumekuja Kwa niaba yake kuwakilisha kiongozi wetu kuja kufariji “amesema.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Itezi, Sambwee Shitambala mbali ya kushukuru kupokea msaada huo ameomba wasisisite kurudi tena kwani bado msaada unahitajika zaidi.
“Uhitaji bado ni mkubwa kwa ndugu zetu hawa tunaomba wadau na watu binafsi kujitokeza kusaidia wenzetu vitu vinavyohitajika ni vikubwa sana ,kuna chakula ,maji ,madawa”amesema Diwani huyo.
Neno la shukrani kwa niaba ya waathirika ilmetolewa na Upendo Mwakasendo ambaye amewashuru wote walioguswa kuwasaidia katika kipindi hiki kigumu wanachopitia kwani wengi wao wamepoteza kila kitu vikiwemo vyakula,mavazi na fedha.
Bado msaada wa kibinadamu unahitajika sana kwa wananchi hao vikiwemo vyakula,nguo na malazi kutokana na wananchi hao baadhi kushindwa kuokoa vitu vyote vilivyokuwemo ndani.
Maporomoko yaliyoambatana na tope lenye uji uji yalitokea wiki iliyopita na kusababisha nyumba 20 na shule moja kufunikwa na tope ambalo limepelekea wananchi kukosa nyumba za kuishi na kuishi shule ya msingi Tambulikareli kwa muda .
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba