Na Esther Macha Timesmajira Online, Mbeya
NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi amewatembelea majeruhi wa ajali iliyohusisha basi la CRN na gari la miundombinu ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya iliyosababisha vifo vya watu wanne na majeruhi watano.

Miongoni mwa majeruhi waliotembelewa katika hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya ni pamoja na Katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya Lucia Sule, Waandishi wa Habari Epmacus Kalokola,Denis George na Seleman Ndelage.
Mhandisi Mahundi akiwa katika hospitali Rufaa kanda ya Mbeya amepongeza uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa namna wanavyopambana kuokoa maisha ya majeruhi hao.
Huku akipongeza Serikali ya awamu kwa kuwekeza vifaa tiba hivyo kuokoa gharama za kwenda hospitali nje ya Mkoa na nje ya nchi.
Wakati ikitokea ajali hiyo Mhandisi Maryprisca Mahundi alikuwa ziara ya kikazi nchini Zimbabwe.

More Stories
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Baraza la Taifa la Ujenzi waingia makubaliano ya mashirikiano sekta ya ujenzi
Nderiananga aongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa tatu wa Kimataifa wa watu wenye ulemavu ujerumani
Taarifa za maendeleo ziwafikie wananchi kwa usahihi