Na Esther Macha, TimesmajiraOnline, Busokelo
MAMA lishe 89 kutoka Halmashauri ya Busokelo na Rungwe Mkoa wa Mbeya wamenufaika na tamasha la Maryprisca Mama Ntilie 2023 la lililozinduliwa Oktoba 4 mwaka huu.
Tamasha hilo ambalo limeratibiwa na Naibu Waziri wa Maji,Mbunge Vitimaalum Wanawake Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi lenye lengo la kuwainua kiuchumi Mama Ntilie wa kipato cha chini.
Akizungumza na Majira,Mhandisi Mahundi amesema kuwa kati ya washiriki 89 watano wamepatiwa mitaji ya sh 30,000 kila mmoja huku mshindi wa kwanza amepata fursa ya kujiendeleza mafunzo ya mapishi na Ujasiriamali katika Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) mkoani
“Lengo ni kuwainua kiuchumi Mama Ntilie wa kiwango cha chini kabisa hivyo kama mwakilishi wao nitapita kila jimbo kugawa majiko ya gesi sambamba na kuwaondoa na matumizi ya Mkaa na kuni nataka ndugu zangu akina mama tubadilike nina njema kabisa nyie nataka tubadilike kiuchumi kabisa”amesema
Wakati huo huo Mahundi ametoa majiko mengine 21 kwa washiriki waliotoka maeneo ya mbali waliofika kushiriki tamasha hilo hadhimu.
Diwani wa Kata ya Ibigi , Lidia Sanga amemtaka Mbunge huyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujali watu wa chini ambao wana kipato duni na kuwasaidia wanawake ili waweze kusonga mbele kiuchumi.
Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Mbeya Suma Fyandomo, amesema kuwa kitendo cha Mhandisi Mahundi alichofanya ni kitu kikubwa sana cha kuwainua wanawake kiuchumi kwa kuwapatia mitaji .
Diwani wa Kata ya Kandete Halmashauri ya Bukokelo ,Botuli Kagenga amesema kuwa Mbunge huyo anafanya utekelezaji na ingekuwa siasa wangejazana wana CCM peke.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi