January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mahakama kuu yafuta Kesi ya kupinga mkataba wa Bandari

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mbeya leo Agosti 10, 2023 imetupilia mbali maombi yote sita ya walalamikaji waliofungua ya kupinga mkataba wa uwekezaji katika Bandari ya Dar es salaam

Walifungua kesi hiyo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na Katibu Mkuu wa wizara hiyo.

Kesi hiyo ilitajwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Julai 3 na ikaanza kusikilizwa Julai 20, mwaka huu.