Na David John, TimesMajira,Online Geita
AFISA Vipimo Mkoa wa Geita, Chrispinus Aloyce, amemshukuru Rais John Magufuli kwa kusogeza huduma kwa wadau zinazohusiana na biashara ya madini.
Amesema kuwa Geita imebarikiwa kuwa na maeneo mengi ya uchimbaji wa madini pia masoko ya madini ya dhahabu, hivyo kuwasogezea huduma hizo kumewaondolea vikwazo mbalimbali wananchi.
Aloyce ameyasema hayo leo kwenye Maonyesho ya Madini yanayoendelea mkoani hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sababu za wao kushiriki maonesho hayo .
“Tunamshukuru Rais Magufuli kwa kwa kusogeza karibu huduma ya biashara hii ya madini ukizingatia Geita ina masoko tisa,”amesema.
Ametaja baadhi ya masoko hayo kuwa ni Geita Mjini, Katoro, Nyang’hwale, Mbogwe pamoja na maeneo mengine ndani ya mkoa wa Geita.
Ameongeza kuwa wao kama Wakala wa Vipimo kazi yao kubwa kukagua na kuhakiki mizani ambayo wafanyabiashara wanaitumia ipo sahihi, hivyo wasiwe na wasiwasi kwani mizani yote inayotumika kupima madini imeshahakikiwa na ipo salama.
“Tunawaalika wadau mbalimbali kutembelea kwenye banda letu kwani kuna mambo mengi ya kujifunza kuhusiana na kazi zetu na kama wanakutana nachangamoto zinazohusu vipimo basi wasisite kutembelea Ofisi za wakala wa Vipimo popote nchini,”amesema Ofisa Mawasiliano wa Vipimo, Paulus Oluochi.
More Stories
Bodaboda wamchangia Rais Samia Mil 1 ya fomu ya Urais
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani