Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
WIZARA ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imesema inajivunia mafanikio makubwa katika awamu zote sita za serikali katika michezo kwenye timu za majeshi yalipo chini ya Wizara hiyo.
Ambapo timu za majeshi zimefanya vizuri ikiwemo mashujaa FC iliyopo mkoani Kigoma kufanikiwa kupanda ligi kuu Tanzania Bara na Kuungana na timu ya JKT Tanzania.
Hayo yamesemwa jijini hapa leo,Aprili 3,2024 na Waziri wa Wizara hiyo Dkt.Stergomena Tax wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika miaka 60 ya muungano.
Pia amesema timu ya wanawake ya mpira wa miguu ya JKT Queens nayo imeendelea kufanya vizuri katika michezo ya ligi kuu ya wanawake na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa CECAFA kwa mwaka 2022/2023 iliyowapa tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika kwa wanawake nchini Ivory Coast.
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM