Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela wamepitisha makadirio ya mapato na matumizi ya mpango wa bajeti ya Mwaka 2024/25 ya kiasi cha bilioni 81.4.
Akiwasilisha muhtasari wa mpango na bajeti ya Mwaka 2024)2025 katika kikao cha Baraza la Madiwani uchambuzi na kupokea mpango na bajeti hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo Februari Mosi,2024 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Herbert Bilia ameeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 makisio ya bajeti inategemea katika maeneo muhimu manne.
“Halmashauri inaomba kuidhinishiwa makisio ya kiasi cha zaidi ya bilioni 81.4 kati ya fedha hizo zaidi ya bilioni 10.06 ni kwa ajili ya ruzuku ya miradi ya maendeleo,zaidi ya bilioni 55.6 ni mishahara,zaidi ya bilioni 1.0 ruzuku ya matumizi ya kawaida na zaidi ya bilioni 14.7ni mapato ya ndani ambapo zaidi ya bilioni 8.0 kati ya fedha hizo ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo zaidi ya bilioni 5.3 ni matumizi ya kawaida na zaidi ya bilioni 1. ni mapato fungwa,”ameeleza Bilia.
Ambapo ameeleza kuwa bajeti ya mishahara imeongezeka kutoka zaidi ya bilioni 43.5 kwa mwaka 2023/2024 hadi zaidi ya bilioni 55.6, kwa mwaka 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 27.6 ongezeko hilo linatokana na ajira mpya, upandishwaji wa madaraja na vyeo kwa watumishi wa kada mbalimbali.
Aidha ametaja vipaumbele vya miradi ya maendeleo kwa mwaka 2024/2025 ni pamoja na sekta ya elimu.
Ambapo katika sekta ya elimu msingi ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa katika shule za msingi Chasubi Kata ya Sangabuye milioni 75,umaliziaji wa madarasa 10 shule ya msingi Igombe Kata ya Bugogwa milioni 90,ununuzi wa samani za ofisi katika shule za msingi milioni 10,ujenzi wa Shule mpya Kata ya Kawekamo milioni 100.
Pia ununuzi wa madawati 200 kwa shule za msingi milioni 16,ukamilishaji wa matundu 28 ya vyoo katika shule za msingi Isanzu 14 Kata ya Bugogwa na Kaselya Kata ya Buswelu14 milioni 30.8,ujenzi wa madarasa 8 (shule Kongwe)katika shule ya msingi Kirumba milioni 200.
Aidha elimu bila malipo kwa shule zaMsingi zaidi ya milioni 946.7,gharama za mitihani ya darasa la nne (SFNA) milioni 375,gharama za mitihani ya darasa la saba(PLSEE) milioni 387,ujenzi wa uzio bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum shule ya msingi Buswelu milioni 30,ujenzi wa darasa 1 la awali na matundu 3 ya vyoo katika shule ya msingi Buzuruga kwa fedha za EP4R milioni 33.5.
Ujenzi wa darasa 1 la awali na matundu 3 ya vyoo katika shule ya msingi Kayenze Ndogo kwa fedha za EP4R milioni 33.5,ujenzi madarasa 6 katika shule za msingi Kayenze ndogo 2, Bwiru 2, na Buzuruga ‘C’ 2 kwa fedha za EP4R milioni 150,ukamilishaji wa nyumba 2 za mwalimu katika shule za msingi Bwiru 1 na Mihama 1 kwa fedha za EP4R milioni 36.
Aidha ujenzi wa vyumba 32 vya madarasa katika shule za msingi Bugungumuki 2,Isesa 2, Kaselya 2, Nyamhongolo 4, Kilimani 2, Kiloleli 2, Lukobe 2, Mnarani 2, Mwambani 2, Nundu D 2, Umoja 2, Isanzu 3, Magaka 3, na Kabangaja 2 kwa fedha za BOOST milioni 725,ujenzi wa darasa 1 la awali na matundu 3 ya vyoo katika shule ya msingi Bezi Kata ya Kayenze kwa fedha za BOOST milioni 33.05.
Ujenzi wa matundu 56 ya vyoo katika shule za msingi Kilabela 14, Nyafula 14, Kiseke 14, na Ziwani 14 kwa fedha za BOOST .milioni 61.6,ukamilishaji wa nyumba 1 katika shule ya msingi Tumaini Kata yaKirumba kwa fedha za BOOST milioni 18,kuwezesha ukamilishaji wa miradi viporo katika sekta ya elimu msingi milioni 180.5.
Upande wa elimu sekondari ni kuwezesha umaliziaji wa bwalo shule ya sekondari Sangabuye milioni 70,kuwezesha ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kata ya Ilemela milioni 584,ujenzi wa shule mpya ya SekondariBusenga Kata ya Buswelu milioni 584,ujenzi wa madarasa 4 na ofisi 1 shule mpya ya sekondari mtaa wa Masemele Kata ya Bugogwa milioni 100.
Pia ununuzi wa viti na meza 200 kwa shule za sekondari milioni 16,ukamilishaji wa miradi viporo katika sekta ya elimu sekondari zaidi ya milioni 145.3,kuwezesha ujenzi wa shule mpya katika Kata ya Mecco kwa fedha zaSEQUIP milioni 570,kuwezesha wanafunzi wasiojiweza kujikimu mahitaji yao kwa fedha zaCAMFED zaidi ya milioni 35.5.
Pia elimu bila malipo kwa shule za sekondari zaidi ya bilioni 2.2,uendeshaji wa shughuli za mitihani ya kidato cha pili, cha nne na cha sita zaidi ya milioni 990.
Sekta ya afya
Bilia ameeleza kuwa katika sekta ya afya ni kuwezesha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje katika Kituo cha afya Kata ya Ibungilo milioni 250,kuwezesha ujenzi wa zahanati mpya Kata ya Kitangiri milioni 70,kuwezesha ujenzi wa zahanati mpya mtaa wa Mecco Mashariki milioni 70.
Pia upanuzi wa zahanati ya Nyamh’ongolo kuwa kituo cha afya milioni 100,kuwezesha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje(OPD) kituo cha afya Kata ya Nyasaka milioni 100,kuwezesha ujenzi wa zahanati ya Bwiru Kata ya Pasiansi milioni 70,ujenzi wa zahanati mpya mtaa wa Kigala milioni 70.
Kuwezesha umaliziaji wa wodi ya mama na mtoto zahanati ya Nyakato milioni 100,kuwezesha ujenzi wa zahanati mpya Ibanda Ziwani Kata ya Kirumba milioni 70,umaliziaji wa jengo la mama na mtoto zahanati ya Luhanga Kata ya Kiseke milioni 40.
Vilevile kuwezesha ukamilishaji wa maabara zahanati ya Kahama milioni 35,ukamilishaji wa miradi viporo sekta ya afya zaidi ya milioni 152,ununuzi wa vifaa tiba, vifaa vya meno, vitendanishi vya uchunguzi kila robo mwaka katika zahanati 7 za Lumala, Masemele, Nyamadoke,Nyambiti, Kawekamo na Bezi milioni 100.
Sanjari na kuwezesha umaliziaji wa zahanati ya Nyambiti milioni 50,uununuzi wa vifaa tiba katika hospitali ya Wilaya kila robo mwaka milioni 500, kununua vifaa tiba, vitendanishi vya uchunguzi kila robo mwaka katika kituo cha afya cha Kayenze milioni 300 na shughuli za Mfuko wa Pamoja wa Afya (HSBF), Global fund, GAVI na wadau wa Afya zaidi ya milioni 925.
Pia ameeleza kuwa sekta nyingine kipaumbele katika mpango na bajeti hiyo ni sekta ya miundombinu ikiwemo ujenzi wa barabara katika kata zote 19 za Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela bilioni 1.1.
Pamoja na udhibiti taka na usafishaji ikiwemo gharama za matengenezo ya magari ya kusafirisha na usimamizi wa taka ngumu zaidi ya milioni 38,kuwezesha matengenezo ya vikapu vidogo 164 (street bins) kwa ajili ya mitaa zaidi ya milioni 19,kuwezesha ujenzi wa ofisi 6 katika maeneo ya makaburi ya umma zaidi ya milioni 47.7 na kuwezesha ujenzi wa eneo la kutupia taka (controll tipping dumping site) milioni 100.
Huku sekta nyingine ni sekta ya maendeleo ya jamii,biashara,viwanda na uwekezaji,kilimo,mifugo na uvuvi,tehama,maliasili na uhifadhi pamoja na utawala.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nyamanoro George Maganiko ameeleza kuridhishwa na mpango wa bajeti hiyo ya mwaka 2024/25 kwani imegusa maeneo yote.
“Kwenye Kata yangu katika bajeti hii nimefanikiwa kupata majengo ya ofisi ya serikali za mitaa pia zahanati nawapongeza waandaaji wa bajeti hii imekidhi viwango na imegusa kila sehemu ikiwemo upande wa shule,afya, miundombinu na vitu vingine,”ameeleza Maganiko.
More Stories
Wassira:Waliopora ardhi za vijiji warudishe kwa wananchi
Rais Samia apongezwa kwa miongozo madhubuti ya ukusanyaji wa kodi
Mwenda:Siku ya shukrani kwa mlipakodi ni maalum kwaajili ya kuwatambua,kuwashukuru