Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
MADIWANI wa VIti Maalum, Wanawake wilaya ya Ilala, Rukia Mwenge ,kwa kushirikiana na Diwani wa Viti Maalum Batuly Mziya, wametoa misaada ya chakula kwa watoto wa Makundi Maalum wanaolelewa na kituo cha Upendo Orphanage Center, kilichopo Buguruni Wilaya ya Ilala.
“Sisi madiwani wa viti Maalum jukumu letu kubwa kusaidia jamii mbali mbali kutatua changamoto zao hasa walio katika mazingira magumu leo na Diwani mwenzangu Batury Mziya, tumegawa vyakula mbalimbali ikiwemo sukari,Unga,Sabuni katika kituo hichi cha Orphanage Center “alisema Rukia .
Diwani Rukia Mwenge, aliitaka jamii kuwa karibu na watoto wa makundi maalum kwa ajili ya kuwasaidia ili na wao wawe na furaha kama watoto wengine.
Diwani wa Viti Maalum Batuly Mziya ,alisema dhumuni kuu la kusaidia watoto wa makundi maalum kuwa karibu na jamii ambapo alisema katika ziara zao madiwani wa viti Maalum wanaongozana na viongozi wa Umoja wanawake UWT .
Diwani Batuly Mziya alisema katika ziara hiyo katika kituo cha watoto yatima kukutana na watoto hao wamefarijika sana watoto hao sawa na watoto wao.
Mlezi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Upendo Orphanage Center, Johari Yusuph ,alisema kituo hicho kimesajiliwa kimeanza kutoa huduma 2001 , kina watoto 30 wa kike 15 na wa kiume 15 wanasoma elimu ya awali na elimu msingi .
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba