Ashura Jumapili TimesMajira online, Bukoba,
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Bukoba limepitisha rasimu ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/26 kiasi cha shilingi bilioni 51.9.
Akisoma rasimu hiyo Februari 12,2025 katika kikao cha Baraza la Madiwani kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bukoba,Mkuu wa Idara ya Mipango Miji,Rahel Mbuta,amesema fedha hizo zitatumika katika shughuli za maendeleo, mishahara,matumizi ya kawaida.

Mbuta,amesema Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26 imekisia kukusanya kiasi cha bilioni 4 kutokana na vyanzo vyake vya mapato ya ndani ikiwa ni ongezeko la asilimia 30 ikilinganishwa na mwaka wa fedha 2024/25, ambapo yamegawanyika katika makundi mawili ambayo ni mapato halisi na mapato fungiwa.
Amesema,wanatarajia kukusanya mapato halisi kiasi cha bilioni 3.3,sawa na ongezeko la asilimia 34 ikilinganishwa na bajeti iliyopita ya mwaka 2024/25,fedha hizo ni kwa ajili ya shughuli mbalimbali za uendeshaji wa Halmashauri na miradi ya maendeleo na fedha za mapato ya ndani fungiwa ni miloni 722.9.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Bukoba Murshid Ngeze,amesema bajeti hiyo imezingatia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)2025 na vipaumbele vilivyoibuliwa na wananchi ikiwemo kuandaa kesho ya Vijana BBT kwa upande wa uvuvi na imegusa zaidi maisha ya wananchi.
Amessema Watendaji wa Vijiji na Kata wamekuwa wakisimamia ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao hivyo kuwataka waendelee kuongeza juhudi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,Erasto Sima,amesema ukusanyaji wa mapato utasaidia katika shughuli za maendeleo huku rasilimali zilizopo hasa mazao ya uvuvi,kilimo na zao la kahawa ziweze kusaidia katika mapato ya ndani.

More Stories
Tanzania,Umoja wa Ulaya kukuza na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara
Serikali yashirikiana na wananchi kujenga shule karibu na makazi Musoma vijijini
Kliniki ya Sheria bila malipo yazinduliwa Mwanza