Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Muheza
Halmashauri ya wilaya ya Muheza Mkoani Tanga imekabidhi madarasa 67 yaliyojengwa kutokana na fedha za Uviko 19 ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 100 ambapo hadi kukamlikia kwa ujenzi huo wa madarasa hayo kutasaidia zaidi ya wananfunzi 1440 kupata nafasi ya kusoma vizuri.
Makabidhiano hayo imefanyika jana katika shule ya sekondari ya Chief Mang’enya na kushirikisha viongozi wa vyama na serikali pamoja na wakuu wa idara na wakuu wa shule.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Muheza Nassibu Mmbaga alikabidhi vyumba hivyo 67 pamoja na madawati kwa mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Muheza Nassibu Mmbaga alisema kuwa halmashauri hiyo ilipata jumla ya shilingi 1,420,000,000 kupitia mradi namba, 5441_TCRP kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 67 vya madarasa ya sekondari ambavyo vimekabidhiwa kwa mkuu wa wilaya ya Muheza.
Alisema kuwa idara ya elimu msingi imepata vyumba vya madarasa 10 vya shule shikizi tatu na bweni 1 kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum ambapo ujenzi umekamilika.
Mmbaga alisema kuwa kwa upande wa sekondari fedha hiyo imesaidia kuondoa upungufu wa vyumba vya madarasa uliokuwepo wa vyumba 25 na sasa wamepata ziada ya vyumba vya madarasa 32 ambavyo vitawezesha wanafunzi wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza 2022.
Alisema kuwa aidha fedha imesaidia kupata viti na meza ambavyo vitatumiwa na wanafunzi hivyo hakuna mwanafunzi atakayekaa chini.
Mmbaga alisema kuwa kwa upande wa shule za msingi imewezesha kujenga bweni 1 la wanafunzi wenye mahitaji maalum ambalo litasaidia watoto wenye mahitaji maalum kupata huduma ya shule kwa karibu.
Alisema kuwa fedha hiyo pia imesaidia ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa katika shule 3 shikizi ambazo zitaweza kuombewa usajili hali ambayo itasaidia kuondoa changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu kufuata shule.
Awali akipokea mradi huo Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo amesema Halmashauri hiyo ilipata kiasi cha fedha shilingi bilioni 1.4ambazo zilitokana na fedha za Uviko -19 ambapo kiasi hicho cha fedha kimekuwa faraja kwa wanamuheza kwa kuweza kuwasaidia wananfunzi kuendelea na elimu wilayani humo.
Bulembo akipokea madarasa hayo na madawati alisema kuwa fedha hizo zimesaidia kupata madawati ambayo yatatumiwa na wanafunzi hivyo hakuna mwanafunzi atakayekaa chini.
Alisema kuwa wilaya ya Muheza wanaishukuru serikali ya awamu ya sita ya rais Samia Suluhu kwa kuleta fedha hizo zimesaidia kuboresha miundombinu ya elimu katika shule za msingi na sekondari.
Bulembo alitoa onyo kwa wazazi ambao watabainika watoto wao hawajawapeleka shule katika wilaya hiyo wakibainika watachukuliwa hatua kali ikiwamo kushtakiwa kwa kuwa serikali imetumia fedha nyingi kujenga madarasa sasa lazima kila mtoto apate elimu.
alitoa rai kwa walimu na wanafunzi wa shule hizo kutunza madarasa hayo mapya ili yadumu kwa muda mrefu kwa kuwa serikali imetoka fedha nyingi katika ujenzi ambao ni fedha za mkopo.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam