December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Madaktari wataka vifaa kukabiliana na Corona

Na Mwandishi Wetu

CHAMA cha Madaktari Tanzania (MAT) kimeiomba Serikali kuhakikisha madaktari na wauguzi wanapatiwa vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) ili wasipate maambukizi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Rais wa MAT, Dkt. Elisha Osati alisema vifaa vya kujikinga na Corona ni muhimu kwao ikizingatiwa idadi ya wagonjwa na walio katika hatari ya kupata maambukizi inaongezeka.

“Tunadhani kuna nguvu inatakiwa kuongezwa, hivyo tahadhari ni muhimu sana kwa sababu dunia nzima wanalia na uhaba wa vifaa,” alisema Dk Osati. Dkt. Osati aliipongeza Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Afya kwa namna wanavyoongoza nchi kupambana na ugonjwa huo.

Alisema juhudi zinazochukuliwa na Serikali wanaziona ni nzuri, lakini zipo changamoto ambazo chache. “Lakini pia tunashukuru madaktari, manesi na watumishi wengine wa sekta ya afya ambao wapo mstari wa mbele kuweza kushughulikia wagonjwa hata wakati wa hatari, kwa sababu wapo mstari wa mbele katika kupambana na huu ugonjwa,” alisema.

Alitoa mwito kwa watumishi wa kada ya afya waendelee kufanyakazi pamoja na changamoto iliyopo. “Hapo sasa ndiyo tunaiomba Serikali na wadau wengine kuhakikisha watumishi wanapewa vifaa vya kutosha kuweza kujikinga vizuri, kwani bila wao kujikinga nao pia watapata maambukizi.

Madaktari wakiambukizwa ni shida kwa sababu tumeona nchi kama Italia madaktari 61 wamepata ugonjwa, hiyo inapunguza nguvu kazi na morali ya wengine kutoa huduma,” alisisitiza, Dkt. Osati .

Dkt. Osati alishauri Serikali kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye kliniki za magonjwa mengine kama kisukari na UKIMWI kwa kutoa dawa za muda mrefu.

“Mfano wagonjwa wale wa kisukari, shinikizo la damu, maumivu migongo na misuli wanaweza kupewa dawa walau za miezi mitatu kwa sababu hawa wana uwezekano wa kupata ugonjwa mkali zaidi,” alisema. Dkt Osati na kuongeza; “Kwa sababu tunajua hawa na magonjwa mengine.” Alisema wanachokiomba Serikali

wenye magonjwa sugu wana uwezekano wa kuambukizwa rahisi ikilinganishwa na wengine, lakini pia wakiambukizwa wanapata ugonjwa mkali na wanakuwa kwenye hatari ya kufa kama tunavyoona kwenye nchini nyingine, wanaofariki kwa wingi zaidi ni wazee, lakini wenye magonjwa mengine na hata huyu aliyefariki hapa kwetu juzi alikuwa

iruhusu kutoa dawa ya miezi mitatu kwa wagonjwa hao kwa sababu sera hairuhusu, labda kwa kibali maalum. “Kwa hiyo tunachokiomba kupitia bima kama za NHIF na nyingine kuweza kuruhusu wagonjwa waweze kupewa dawa za muda mrefu ili kama hana sababu ya kuja hospitali, sio lazima aje,” alisema.