Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Hayo yalisemwa na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa Mkoa Amana Dkt.Bryson Kiwelu katika madhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambapo alishiriki siku hiyo na Watumishi wake Wanawake.
Dkt.Bryson Kiwelu alisema Wanawake ni nguzo muhimu katika familia pia ni watendaji katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
“Katika hospitali yetu ya Rufaa Mkoa Amana asilimia 70 Wauguzi wetu wanaotoa huduma wakiwemo madaktari ni Wanawake na Leo ni siku muhimu ya Wanawake Duniani huduma zote zinatolewa Bure Kwa Siku ya Leo na madaktari Wanawake nawaomba Wananchi wa Wilaya ya Ilala na pembezoni mfike kupata huduma Bure asubuhi mpaka jioni”alisema Dkt.Kiwelu
Dkt Kiwelu alisema huduma zote siku ya Leo zinatolewa na wauguzi na madaktari Wanawake kutibu magonjwa mbalimbali .
Aidha Dkt.Kiwelu alisema mikakati ya hospitali hiyo kujenga jengo la kisasa la kusafisha damu michakato yake imeanza rasmi.
Pia alisema mikakati mingine wanajenga Jengo la wagonjwa Maalum ambalo litatoa huduma za kisasa.
Kwa upande wake Dkt Bingwa,wa magonjwa ya Masikio pua na Koo
Fatuma Kibao alisema Leo siku yao Maalum Wanawake wamejitoa katika madhimisho hayo kusaidia Jamii katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika sekta ya Afya.
Fatuma kibao alisema katika hutoaji wa Huduma za Afya Leo wanatibu wagonjwa wa magonjwa mbalimbali yakiwemo nyemelezi.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote