Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
MADAKTARI bingwa wa upasuaji wa ubongo wameendelea kuongezeka katika Taasisi ya Mifupa (MOI) na kufikia 16 hali ambayo imeendelea kuifanya Tanzania kuwa kivutio cha utalii tiba Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Madaktari hao walikuwa India kwa siku 10 wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Utalii Tifa Taifa, ambaye ni Mkurugenzi wa Global Education Link na Global Medicare, Abdulmalik.
Mollel amepewa ruhusa na Mwenyekiti wake, Profresa Mohamed Janabi ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, (MNH) kuongozana na ujumbe huo .
Hayo yamesemwa jana jijjini Dar es Salaam na daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mgongo wa taasisi hiyo, Nicephorus Rutabasibwa, wakati akizungumza kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Terminal III.
Akizungumza wakati yeye na madaktari bingwa 10 waliporejea kutoka India ambapo walikwenda kutafuta fursa za kushirikiana na hospitali mbalimbali za nchini humo ikiwa ni jitihada za kukuza utalii tiba hapa nchini.
Amesema waliangalia nguvu ya Tanzania katika matibabu na kwamba hawakukuta tofauti sana kwani vifaa tiba na rasilimali watu ya madaktari iliyoko kule ni kama iliyoko hapa nchini.
“Wana vifaa vya kufanyia upasuaji ambavyo nasisi tunavyo, wanavifaa vya kufanyia uchunguzi kama MRI na ST SCAN ambavyo nasisi tunavyo kitu kipya ni matumizi ya roboti ambayo hawana hata miaka mitano nasisi tutajipanga kufikia huko. Tumeangalia fursa za kushirikiana nao katika kufundisha madaktari ,” amesema
Aidha, serikali ya awamu ya sita imewekeza vifaa vya kisasa na rasilimali watu kwenye taasisi hiyo hivyo kuweza kumudu kufanya upasuaji wa teknolojia ya hali ya juu kama ilivyo India.
“Waambieni watanzania na waafrika wengine kwamba mtu mwenye shida ya upasuaji wa ubongo au upasuaji wa aina yoyote wa mifupa halazimiki tena kwenda India anaweza kuja MOI mambo yakaenda vizuri kabisa na akaokoa gharama,” amesema
Kwa upande wake, taasisi ya saratani ya Oceanroad (ORCI), imesema inauwezo wa kufanya utalii wa tiba Afrika kutokana na kuwa na vifaa tiba vya kisasa na madaktari bingwa wa kutosha kama ilivyo mataifa mengine kama India.
Daktari bingwa wa saratani wa taasisi hiyo, Dk Calorine Swai, ambaye ni daktari bingwa ya saratani Taasisi hiyo, ameyasema hayo aliporejea na ujumbe wa madaktari bingwa 10 kutoka Indiaa ambako walikwendaa kuangalia fursa.
Madaktari hao walikwenda India ambako walikaa kwa siku 10 wakiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Utalii Tifa, Abdulmalik Molle, kuangalia namna ya kushirikiana na hospitali hizo katika utalii tiba.
Amesema kwa upande wa vifaa vya matibabu na madaktari bingwa aliowashuhudia nchini humo ni kama waliopo kwenye taasisi hiyo hivyo wana uhakika wagonjwa kutoka mataifa mengi Afrika wanaweza kuja ORCI na kupata tiba kamili.
“Tofauti ndogo niliyoona ni kuwa na viwanda vingi vya kutengeneza vifaa tiba na dawa za saratani na hali hiyo imeifanya huduma ya saratani kwao kuwa rahisi sana kupatikana kila inapohitajika. Tumeona mashine ya mionzi waliyonayo wenzetu imekwenda mbele kwa teknolojia ya kisasa lakini tutafika,” amesema
Amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa anaoendelea kuufanya kwenye sekta ya afya kwa ununuzi wa vifaa tiba na kuajiri wataalamu wabobezi kwamba ndio kunaifanya Tanzania kuanza kuwa kivutio cha utalii tiba Afrika.
Naye Mollel amesema ujumbe huo ulikuwa unatafuta wabia muhimu je ni nani katika wabia hawa yuko mamkini kufanya naye kazi katika uboreshaji wa huduma za afya zitakazovutia nchi jirani kuona Tanznaia kama kituo muhimu cha kupata tiba.
Molle pia amesema waliangalia fursa kwaajili ya kuwajengea uwezo wataalamu wa tiba Tanzania kwenye sekta ya afya na kwamba miongoni mwa mafanikio makubwa waliyopata ni kufika kwenye miji mikubwa mitatu nchini India ambayo imefanikiwa sana katika utalii tiba duniani.
“Tulianzia mji wa Hyderabad ambapo tulikaa siku nne tukaenda Bangarole na kisha tukahamia mji wa New Delhi na katika miji hiyo tumepitia hospitali nyingi na wadau wengi wa afya kujifunza kuhusu upatikanaji wagonjwa kutoka nje ya nchi, teknolojia zipi zitumike,” amesema Mollel na kuongeza
“Huwezi ukazungumzia utalii tiba bila kutaja hospitali kama Apollo ambao imeshafanyakazi hii kwa miaka zaidi ya 20, pia tulienda hospitali kama BLK, Fortis, Medanta, Yashoda, Rainbow ambayo ni maalum kwa watoto wadogo na HCG ambayo imebobea kwenye saratani,” amesema
Amesema hospitali ya Yashoda ni kundi la hospitali nne zenye jumla ya vitanda 4,000 wakati HCG ni kundi la hospitali 24, Rainbow kundi la hospitali kama 17 na mtandao wa Hospitali za Appolo wenye hospitali 70 na Fortis yenye hospitali 10 na vituo vya afya chini yake.
Amesema hospitali zote walizotembelea ndizo kwa kiwango kikubwa zimechangia mapinduzi makubwa kwenye utalii tiba nchini India kwa kushirikiana na serikali yao na kwamba ziliwapokea vizuri na kuunga mkono na kupongeza mtazamo wa serikali ya Tanzania kutaka kuipaisha kwenye huduma za afya duniani.
“Walitupokea vizuri na wakaipongeza Tanzania kwamba imekuwa na uhusiano mzuri sana na India na inatoa huduma kwa kushirikiana na mataifa mbalimabli ikiwemo India kwenye sekta ya afya na imekuwa kimbilio la watu wengi wakiwemo wawekezaji walisema ni nchi ya amani na kimbilio la watalii wa kawaida kwa hiyo hili ni jambo jema,” amesema
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba