December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mabula awataka Watanzania kuchapa kazi 2023

DKT MABULA AWATAKA WATANZANIA KUTUMIA MWAKA 2023 KWA KUCHAPA KAZI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula amewatakia watanzania heri ya mwaka mpya 2023 na kuwataka kutumia mwaka huo kuchapa kazi kwa bidii ili kuliletea taifa maendeleo.

Dkt Mabula alitumia maadhimisho ya mwaka mpya usiku wa kuamkia tarehe 1 Januari 2023 nyumbani kwa Dar es Salaam kwa kutoa rai kwa watanzania wote kuutumia mwaka wa 2023 kufanya kazi kwa bidii huku wakiwa na hofu ya Mungu.

“Rai yangu katika mwaka huu mpya wa 2023 ni mwaka wa sala na kazi, tukatende kazi tukiwa na hofu ya mungu tukatumikie watanzania taifa linatutegemea kila la kheri watanzania wote Mungu awabariki sana” Dkt Angeline Mabula.