Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online, Dar
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, leo Jijini Dar es Salaam, amewasihi watu wanaoshiriki kwenye maandamano yanayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kufanya maandamano yanayolinda uwekezaji uliofanywa katika Jiji la Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa mapema leo Jijini humo na Mkuu wa mkuo huyo, wakati akiendelea na zoezi la usafi katika maeneo ya Mbezi Mwisho, usafi aliotangaza kufanyika kwa siku mbili Jijini humo ambao ulianza jana, wenye lengo la kujikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Kipindupindu.
Chalamila, akiendelea na shughuli za usafi, amekutana na watu walioshiriki maandamano ya CHADEMA, ambapo amesema ” Dar es Salaam ndipo Vilipo Viwanda vingi, ndipo kuna hospitali kubwa, mzungumko mkubwa wa fedha na Uwekezaji, kwahiyo maandamano yetu yanapaswa kulinda huo uwekezaji ambao nchi imefanya..kwa sababu watoto wako wewe, watoto wangu na mimi na wewe tutafaidika na huo uwekezaji hivyo tukipaharibu dar es salaam hatuna pa kukimbilia”, amesema Chalamila.
Aidha, amewatoa hofu waandamanaji hao, kwa kuwataka kufikisha ujumbe wao sehemu inayostahiri, kwa kudai kuwa Serikali imeridhia kuwepo kwa maandamano hayo ya amani.
” Rais na viongozi wote wamesema acha watu waandamane wafikishwa ujumbe wao panapostahili, huku pia tukiamini kwamba CHADEMA kama chama kikubwa katika nchi yetu, CCM na Vyama vingine vyote hatupaswi kuhitilafiana kwa itikadi za Vyama vyetu na Mimi RC wenu naendelea na usafi kwa sababu Sasa hivi kuna mlipuko wa magonjwa makubwa hivyo tunaendelea kufanya usafi na nyinyi endeleeni na kufikisha ujumbe kwa jamii mliyoikusudia”, amesema Chalamila.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua