December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina alipokuwa akikagua katika shirika linaotayarisha dawa ya Corona.

Maambukizi Corona yapanda Madagascar, yaweka amri ya kutotoka nje

Na Jacque Mkota, TimesMajira Online

Kufuatia ongezeko jipya la maambukizi ya virusi vya corona nchini Madagascar, Rais wa nchi hiyo Andry Rajoelina aimeuwekea mji wake mkuu Antananarivo amri ya kutotoka nje kwa muda wa miezi miwili baada ya masharti hayo kuondolewa.

Akizungumzia suala hilo Rais Rajoelina amesema, eneo la Analamanga ambalo ndilo lenye mji mkuu linafungwa tena na kuzuia magari kuingia wala kutoka.

  ”Hakuna magari yatakayoruhusiwa kuingia ama kutoka katika eneo hilo kuanzia leo Jumatatu hadi Julai 20 na masharti makali yatawekwa kwa wanaotoka”

”Ni mtu mmoja mmoja katika kila familia ndiye atakayeruhusiwa kwenda barabarani kati ya saa kumi na mbili asubuhi na saa sita mchana”.   

 Aidha Rais Rajoelina ametaka wanafunzi wapewe kinywaji hicho kwa kiwango kidogo kila baada ya muda kwa siku. 

Madagascar ilikuwa ikiandikisha visa vichache kwa siku vya ugonjwa huo lakini sasa Taifa hilo katika siku za hivi karibuni limethibitisha kuwepo na idadi kubwa ya wagonjwa wa Covid 19 kila siku , ambapo wagonjwa 216 waliripotiwa siku ya Jumamosi baada ya watu 675 kupimwa. 

Aprili , rais Andry Rajaoelina alizindua dawa ya mitishamba ambayo alidai inazuia na kuponya virusi hivyo vya corona.