December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad

Maalim Seif amponza kiongozi NLD

Na Holiness Ulomi, TimesMajira Online

CHAMA cha National League for Democracy (NLD) kimemsimamisha Uongozi aliyekuwa Makamu Mwenyekiti kwa upande wa Zanzibar Ahamed Hamad kwa kukiuka Katiba, Kanuni za Chama cha NLD na sheria ya Vyama vya Siasa.

Uongozi huo umefikia maamuzi hayo baada ya Oktoba 13, 2020 kuonekana katika mkutano wa Kampeni za Chama cha ACT Wazalendo uliofanyika katika Viwanja vya Jadida, Pemba akimnadi mgombea wa uraisi wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad huku akijua wazi kuwa alishiriki katika Mkutano Mkuu wa chama chake cha NLD uliofanyika Agosti 16, 2020 Dar es Salaam wa kumchgua mgombea urais wa NDL upande wa Zanzibar, Mfaume Khamis Hassan.

“Kamati Kuu ya NLD kupitia kikao chake kilichofanyika Dar es Salaam Oktoba 18 kiliazia kumsimamisha uongozi kwa nafasi yake kama Makamu Mwenyekiti Zanzibar mpaka mkutano mkuu utakaofanyika mwaka 2023 hivyo anatakiwa kutojihisha tena kufanya kampeni ya mgombea wa ngazi yoyote ile ya chama kingine cha siasa kwa sababu NLD inaheshimu Katiba yake na sheria ya vyama vya siasa na yeye bado ni mwanachama wa NLD,” iliweka wazi taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari.

Pia taarifa hiyo imesema kuwa, hatakiwi kwenda kwenye mikutano ya vyana vingine vya siasa kwa kukaa au kuhudhuria mikutano kwani kufanya hivyo itakuwa ni sehemu ya kufanya kampeni na endapo atakiuka agizo hilo, hatua kali zaidi zitachukuliwa dhidi yakeikiwemo kusimamishwa uanachama hadi 2023.

“NLD ni taasisi na maamuzi yake yanapita kwenye vikao halali vya chama si vinginevyo na kusisitiza Amani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 kwani ni lulu aliyoiacha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere,”.