Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad akamilisha ziara yake iliyoanza tarehe Julai 29, mwaka huu Kisiwani Pemba.
Zara hiyo ambayo mbali na shughuli nyengine za kuangalia uhai wa chama, kiongozi huyo alikuwa na jukumu ya kuzibadilisha kamati za uongozi za majimbo na mikoa kuwa kamati maalum za ushindi kuelekea uchaguzi mkuu wa October 2020.
Kabla ya kukamilisha ziara yake katika mkoa wa Mjini Unguja kichama, Maalim Seif mapema leo asubuhi amerudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Uraisi wa Zanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo.
Ameweka wazi kwamba kwa upande wa Zanzibar chama kimejiimarisha sana na wanaomba kwa hamu kubwa uchaguzi ufike.
“Nimerudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kuwa mgombea Uraisi kupitia chama changu cha ACT Wazalendo, na kama chetu kitanipitisha kuwa mgombea basi nasema wazi CCM Zanzibar wajiandae na anguko kubwa la fedheha,kwa uimara huu wa chama chetu, CCM Zanzibar tutawashida mara nne zaidi ya kura tulizowashinda mwaka 2015.
Baada ya zoezi hilo Maalim Seif amekutana na kufanya kikao cha ndani na viongozi wa Matawi,Majimbo na Mkoa pamoja na Ngome za chama wa mkoa wa Mjini Unguja kwaajili ya kukamilisha ziara yake kikao kilichofanyika Vuga mjini Unguja.
Kaimu Naibu katibu mkuu ACT Wazalendo Zanzibar Ndugu Salim Bimani ametuma salamu kwa jeshi la Polisi Zanzibar kwakulitaka litende haki,
“Kama Polisi wameweza kufunga barabara kwa ajili ya CCM kwenda kumpokea mgombea wao, basi ikifika zamu yetu na sisi tusije tukazuiwa ili haki itendeke” amesema
Akizungumza na Viongozi wa mkoa wa Mjini, Maalim amewasisitiza wahakikishe wanachama wenyesifa wakiwemo Wanawake na Vijana wanajitokeza kwa wingi kugombea nafasi za udiwani,uwakilishi, ubunge,urais wa Zanzibar pamoja na Urais wa Jamuhuri ya Muungano kwani Chama cha ACT Wazalendo ni chama cha Kidemokrasia na mambo yoye yatakwenda kwa uhuru na uwazi mkubwa.
Maalim Seif amewaeleza wanachama wa chama cha ACT Wazalendo kwamba kazi ndogo iliyobaki kwao kwa sasa ni kulinda ushindi wa chama chao kwani kwa mgombea wa Uraisi ambae Halmashauri kuu ya CCM wamemshusha ni wazi ACT Wazalendo watashinda mapema sana kuliko siku zote.
Mwisho kabisa Maalim Seif ametoa taarifa rasmi ya kumpokea Waziri mkuu mstaafu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambae atajiunga nachama cha ACT Wazalendo kesho tarehe 16/07/2020 Mlimani City Dar es salaam.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
27 kulipwa kifuta jasho Nkasi
Mwakilishi Mkazi wa UN nchini awasilisha hati