December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Lugalo Gofu kumuenzi Mkuu wa Majeshi”NMB CDF TROPHY 2023″

Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam

Shindano la Mchezo wa Gofu la Kumuenzi Mkuu wa Majeshi “NMB CDF TROPHY 2023” linatarajiwa kufanyika rasmi Septemba 2 na 3 Mwaka huu katika Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Lugalo Dar es Salaam.

Akizunguza katika Mkutano wa Waandishi wa Habari Mwenyekiti Wa Lugalo Gofu Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amesema,Mbali na Shindano hilo kumuenzi Mkuu wa Majeshi vilevile litatumika kuenzi siku ya kuzaliwa Kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ.

Kwa Upande Meja Japhet Masai Nahodha wa Lugalo Gofu amesema, shindano hilo kitakuwa la Mikwaju (Gross) na kuhusiha makundi yote wakiwemo Wachezaji wa Kulipwa,watoto,Wazee na wanawake.

Naye Girman Kasiga Mwenyekiti Wa Chama Cha Mchezo wa Gofu nchini (TGU) amesema, kupitia Lugalo Mchezo wa Gofu unakuwa siku Hadi siku hivyo wao kama viongozi wa mchezo huo wataendelea kushirikiana na Wadhamini wa Mchezo huo Ili uweze kufika mbali zaidi.

Kwa Upande wake Mkuu wa Idara wa Wateja Binafsi Aikansia Muro kutoka Benki ya NMB ambao ni Wadhamini wakuu Wa Shindano hilo amesema,anaishukuru Lugalo Gofu Kwa kuwapa nafasi ya kuwa Wadhamini wakuu Wa Shindano Kwa Mika nane Mfululizo ikiwa ni Miongoni mwa Njia za kuwafikia Watanzania.

Wachezaji zaidi ya 100 kutoka Klabu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania wamethibisha Kushiriki Shindano Hilo TPC Moshi, Arusha Gymkhana, Kili Golf, Morogoro Gymkhana,Wenyeji Lugalo Gofu bila kusahau timu ya Jeshi na Raia kutoka nchini Malawi.