Na Joyce Kasiki,Timesmajira Online,Dodoma
TAASISI ya Uanasheria kwa Vitendo (LST) inawakaribisha wananchi kwenye banda lao kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria nchini iliyoanza leo Januari 22 mwaka huu ambayo yanatarajiwa kuhitimishwa Februari Mosi mwaka huu ili waweze kupata msaada wa kisheria.
Akizungumza na waandishi wa habari katika banda hilo kwenye uwanja wa Nyerere maarufu Nyerere Square’,Afisa Mawasiliano wa Taasisi hiyo Fatma Salum amesema,taasisi hiyo inatoa msaada wa kisheria bure hivyo ni vyema wananchi watembelee banda lao la kupata msaada huo katika mambo mbalimbali ya kisheria.
“Tumekuja kwenye maonyesho haya kwa lengo la kuwaonyesha wananchi shughuli zetu lakini pia tunatoa msaada wa kisheria bure hivyo tunawakaribisha wananchi watembelee banda letu hapa Nyerere Square.”amesema Fatma
Kuhusu mafunzo yanayotolewa na Taasisi hiyo Fatma amesema,wanatoa mafunzo ya weledi kwa vitendo kwa wanafunzi ambao wamehitimu shahada ya sheria katika vyuo mbalimbali ambao wanatarajia kuwa watumishi wa umma lakini pia kwa wanaojitegemea.
Aidha amesema kuwa licha ya kutoa mafunzo ya weledi kwa vitendo kwa wahitimu wa shahada ya sheria ,taasisi hiyo pia mwaka jana imeanzisha kozi ya weledi kwa ngazi ya cheti kwa wasaidizi wa kisheria.
“Pamoja na kutoa mafunzo lakini pia tuna kituo cha msaada wa kisheria huduma ambayo tunaitoa bure kwa wanaohitaji .
Maadhimisho wa wiki ya Sheria yamezinduliwa na Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango Januari 22,2023 huku yakipangwa kuhitimishwa Februari Mosi mwaka huu ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakani
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best