March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

LRCT kuendelea na tafiti saba za marekebisho ya sheria

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online

SERIKALI kupitia Tume ya kurekebisha sheria Tanzania (LRCT), imesema kwa sasa inaendelea na tafiti saba za marekebisho ya sheria,ikiwemo sheria inayosimamia maadili,michezo ya kubahatisha ,makosa ya jinai pamoja na sheria zinazo angazia ukuaji wa uchumi.

Akizungunza wakati alipo tembelea na kushuhudia utoaji wa elimu ya marekebisho ya sheria na utendaji wa tume hiyo Katibu Mtendaji wa LRCT, George Nandepo, amesema, hatua hiyo inakuja baada ya tume hiyo kukamilisha tafiti 13 za marekebisho ya sheria zikiwemo za uwekezaji, kilimo pamoja na masuala mbalimbali ambayo wananchi walitoa maoni.

George amesema,watanzania wana nafasi ya kuwasilisha maoni yao juu ya marekebisho ya sheria mbalimbali kupitia njia ya barua na kufikisha maoni hayo katika tume ili kupata sheria ambazo zitajibu na kutatua changanoto katika jamii.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Sheria kutoka tume hiyo, Zainab Issa na baadhi ya wananchi waliohudhuria maonesho ya Saba Saba,wamesema, bado kiwango cha watanzania wanao elewa sheria si cha kuridhisha hivyo jitihada zinahitajika ili kuendelea kutoa elimu ya sheria.