November 6, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Lissu atiwa hatiani kwa uchochezi

Na.Mwandishi Wetu,TimesMajira

MAHAKAMA Kuu Masijala Ndogo ya Dar es Salaam imesema Upande wa Mashtaka umeshindwa kuthibitisha kosa la uhaini katika kesi iliyokuwa ikimkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Taifa Tundu Lissu.

Jaji kiongozi wa kesi Hiyo Danstan Ndunguru ameeleza Mahakamani hapo leo Novemba 6,2026 jijini kwamba ushahidi uliotolewa na Jamuhuri haujaonesha ni kwa namna gani Mshitakiwa alipanga kuzuia uchaguzi na kuhamasisha Uasi.

Jaji Dasntan Nduguru amedai kwamba ushahidi uliokuwa umetolewa na Mashahidi 6 wa Jamuhuri kuanzia namba 4, 5, 8, 11, 13 na namba 14 hauna mashiko juu ya shitaka la Uhaini.

Kutoka na hatua hiyo Mahakama imetupilia mbali kesi ya Uhaini.