December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Lissu Hakamatiki Urais Chadema

Na Mwandishi wetu ,TimesMajira,Online

MATOKEO ya Kura za maoni kwa nafasi ya Urais wa Jamuhuri  ya Muungano wa Tanzania kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA )yametangazwa rasmi na Tundu Lissu kushinda nafasi hiyo kwa kura 405.

Katika kikao kilichokaliwa leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam na Baraza kuu la Chadema limeweza kupiga kura na kumchagua Lissu kushika fimbo ya urais kwa Chama hicho.

Wengine waliogombea na Lissu ni Lazaro Nyalandu ambae amepata kura 36 na Dkt Maryrose Mjinge amepata kura moja.