December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Linah ampa makavu Harmonize

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva kwa upande wa wanawake Linah Sanga, amemchana msanii na Bosi wa Kondegang Rajabu Abdul maarufu kama ‘Harmonize’ kuwa aache mara moja kumfuatilia kwani hamtaki hata kumuona.

Akiweka wazi hilo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagra, baada ya kuona Harmonize anataka kumletea mazoea na ‘kuziingiza’ za chinichini, Linah amesema hamtaki na akome kumfuatilia.

Linah amemchana bosi huyo wa Kondegangs anayetamba na ngoma yake ‘Sandakalawe’ kuwa ameharibu familia ya Kajala na mwanawe Paula halafu anataka kumharibia na yeye kwa kujisogeza kwenye himaya yake.

“Nilianza Safari yangu ya Mziki bila ya hizo kiki Wala Drama. Mashabiki zangu Walinipenda Mimi kupitia Mziki Wangu. Na pia mziki wangu huo huo umekua ukinitangaza bila ya hizo kiki wala Drama, Ila inapofika mahali naona nakosewa heshima siwezi kukaa kimya Kamwe,” amesema Linah.