Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MASHINDANO ya Ligi Kuu ya Kikapu visiwani Zanzibar msimu wa mwaka 2021 yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 20, 2021.
Ligi hiyo itaanza kwa Ligi Kanda ya Unguja na Ligi Kanda Pemba na baada ya kupata timu nne za mwanzo kwa kila Kanda itachezwa hatua ya Nane Bora.
Katika michuano hiyo, timu ambazo zitachuana kwa upande wa Kanda Unguja ni Usolo, Stone Town, A. Magic, mabingwa watetezi Polisi, Nyuki, New West, Milenium na J.k.U huku kwa upande wa wanawake zipo timu za K.V.Z, mabingwa watetezi J.K.U, Zimamoto, New West na A. Magic.
Zitakazoshiriki Ligi kanda Pemba ni Tornado, Clickers, California, Dolphins, A.B.C,
Kichungwani Blezz na Majenz wakati kwa upande wa Wanawake zipo Wete Star na Chake chake Star.
Ligi hiyo ya Kanda itachezwa kwa mfumo wa Ligi ambapo kila timu itacheza na mwenzake na tarehe rasmi yakuanza Ligi Kuu Kanda ya Pemba itatoka baada yakufanya kikao na viongozi wa klabu siku chache zijazo.
Kwa upande wa Ligi B, yenyewe inatarajiwa kuanza sambamba na Ligi hiyo ikishirikisha timu za Sixer’s, Beit el Ra’s, Cavarious, Good Morning, Mbuyuni, Rangers pamoja na Mwembe Tanga.
Timu hizi pia zitacheza kwa mfumo wa Ligi, ambapo timu mbili za juu zitapanda Daraja kuchukua nafasi ya zile zitakazoshuka.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Zanzibar (BAZA), Rashid Hamza Khamis ameuambia Mtandao huu kuwa, tayari fomu za usajili na uhamisho wa Ligi hiyo zimeshaanza kutolewa ambapo mwisho ya kuchukua ni Desemba 30 ambapo zoezi la kurudisha litafungwa rasmi Januari 10 ikiwa ni siku 10 kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Kuongozi huyo amesema kuwa, baada ya kuweka wazi tarehe hiyo ya mashindano ni matumaini yao kuwa, klabu zote zitaanza maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo ili kuongeza ushindano utakaofanya ligi hiyo kuwa bora zaidi.
More Stories
Watumishi wa Fahari wafanya Bonanza
Rais Samia atia mkono mchezo wa masumbwi Tanzania
Chino bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship