Na Angela Mazula, TimesMajira Online
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),kinatambua nia ya Rais Dkt.John Magufuli ya kutotekeleza adhabu ya kifo kwa kuweka wazi wakati akimuapisha jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma tangu miaka mitatu iliyopita.
Akizungumza wakati maadhimisho ya 18 ya kupinga adhabu ya kifo yaliyofanyika Dar es Salaam Mkurugenzi wa kituo hicho Anna Henga amesema kuwa
jamii inahitaji uelewa mpana kubainisha zaidi waathirika wa adhabu ya kifo kwa kuwa wengine wanapata adhabu hiyo bila kuwa na hatia.
Henga amesema kwa Tanzania kuna wahalifu zaidi 400 ambao wanasubiri hukumu ya adhabu kifo ingawa hadi sasa hakuna idadi ya wahalifu kuonyesha kupungua licha ya kuwepo kwa adhabu hiyo ingawa ipo nchini.
“Nchi nyingi dunia zimeendelea kuondoa adhabu ya kifo na kuacha kutekeleza adhabu kwani haina maslahi kwa taifa kwani haijawahi kuleta mabadiliko yeyote,’ amesema Henga.
Naye Mwakilishi wa Beljium hapa nchini Peter Van Achen amesema Serikali ya Beljium inapingana na hukumu ya kifo katika nyanja zote, na hii ni kwa sababu tu ya kufuta kanuni zilizowekwa.
Aidha amesema kwa upande wa Beljium tangu mwaka 1963 haijawahi kutoa hukumu hiyo ya kifo hadi kufikia mwaka 1996 hukumu ya kifo ilipoondolewa kisheria na kutoruhusu uhalifu wa namna yeyote, na hukumu ya kifo kutokupewa kipaumbele kwa nchi za Ubeligiji,Urafasa,Uswizi na katika nchi zote za Umoja wa Mataifa.
Hata hivyo “Tumeamua kuungana na duniani na Mashirika siyo ya kiserikali zaidi 150 ,Serikali za Mitaa na taasisi zote zinazoshughulika na haki za binadamu wote kuwa na kauli moja ya kupinga hukumu ya kifo, kwani bado mpaka sasa hukumu hii inaendelea kwenye baadhi ya sehemu mbalimbali duniani.
Naibu Mkuu Kitengo cha Mipango kutoka Ubalozi wa Ufaransa Alexandre Peaudeau amesema kwa Ufaransa wameondoka hukumu hii ya kifo tangu miaka 39 iliyopita na hukumu ya mara mwisho kutoka nchini humo ilikuwa katika miaka ya sabini,na
kwenye katiba ya nchi hiyo imeweka kipingele cha kutokuwepo hukumu hiyo ya kifo.
Naye mwakilishi kutoka ubalozi wa Uswizi hapa nchini Didier Chassot amesema, nchi yangu ipo kinyume kabisa na hukumu hii ya kifo na sehemu yeyote duniani katika hali yeyote ya kuwa mwandamu asinyongwe kwa kutafuta haki.
Jumla ya nchi 142 ziliondolewa adhabu hiyo au kuacha kuitekeleza kwa upande wa Afrika takribani nchi 20 za kusini mwa Jangwa la Sahara zimeondolewa adhabu hiyo ikiwemo Guinea Bissau, Djibout, Afrika ya Kusini, Senegal, Rwanda, Burundi, Togo, Gabon na Congo Brazavile ni 84 asilimia ya adhabu ya kifo zilizotekelezwa zilitelekezwa katika nchi 4 tuu duniani.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba