Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mkurugenzi Mtendaji wa LG Global Asema Soko la Afrika Mashariki Linakua
Afanya ziara ya kipekee Afrika Mashariki tangu kuteuliwa kwake Disemaba mwaka 2021
Aomba Afrika Mashariki kuunga mkono azma ya Busan ya kuwa mwenyeji wa World Expo 2030
Mkurugenzi Mtendaji wa LG Electronics (LG) bwana William Cho, amesisitiza kwamba kampuni hiyo itaendelea kuimarisha shughuli zake za kibiashara Afrika Mashariki, Kama sehemu ya jitihada zake za kukuza mauzo na mapato katika masoko mapya.
Hatua hii imekuja baada ya maamuzi ya kampuni hiyo ambayo mauzo yake ulimwenguni yanazidi zaidi ya Dola bilioni 63 kwa mwaka 2021, kutafuta kukuza soko lake katika kanda hii ya Afrika Mashariki ambayo imeonekana kukua kwa kasi zaidi kiuchumi duniani, ambayo ina idadi ya watu takribani milioni 284.
Mkurugenzi Mtendaji alibainisha kwamba Afrika Mashariki ni soko ambalo linaonesha matarajio makubwa kufuatia misingi imara ya kiuchumi ambayo inaimarishwa na ina idadi kuwa ya vijana, ukuaji wa kasi wa tabaka la kati maeneo ya mijini, na uwekezaji katika miundombinu na sekta zaingine za muhimu za uchumi.
“Tunaona kuna fursa kubwa katika soko hili na hivyo tutaendelea kuimarisha mahusiano yetu ya kibiashara na nchi zilizoko katika ukanda huu,” alisema bwana Cho.
Alisema haya wakati akitembelea Tanzania, ambako alikutana na watendaji wakuu wa serikali wakiongozwa na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, ambako aliahidi utayari wa kampuni hiyo katika kuongeza usambawaji na mtandao wa wateja wadogo wadogo kwa dhumuni la kusaidia ukuaji wa jamii za chini na uchumi kwa ujumla. Hii ni ziara ya kwanza kwa Mkurugenzi Mtendaji bwana Cho kutembelea Afrika Mashariki tangu kuteuliwa kwake Disemba mwaka 2021.
Wakati wa ziara bwana Cho vile vile alihamasisha kuunga mkono mpango wa Korea kuwa mwenyeji wa Maonyesho ya Kibiashara ya Kimataifa mwaka 2030 (Wold Expo 2030) Jijini Busan, Jiji la pili kwa ukubwa nchini humo.
Korea inaharakisha azma yake ya kuwa mwenyeji wa maonyesho ya kimataifa ya biashara 2030, (World Expo 2030) kabla ya kura kupigwa, ambazo zinatarajiwa kupigwa Novemba 2023 na nchi 170 wanachama wa Bureau Internationale de Expositions, Shirika la kimataifa ambalo linasimamia tukio hilo.
Majiji mengine ambayo yameonyesha azma ya kuwa mwenyeji wa maonyesho hayo ya kibiashara ni Moscow, Riyadh, Odessa na Rome.
“Tuna matumaini kwamba Korea itakuwa mwenyeji wa tukio hili muhimu la kimataifa, ambalo vile vile ni fursa ya kufikiri na kutafuta masuluhisho ya changamoto zinazokabili ulimwengu.Kama kampuni, tunashirikiana na serikali ya Jamhuri ya Korea katika kujenga uungaji mkono wa kimataifa kwa zabuni ya Busan” Alisema bwana Cho.
Waziri Mkuu wa Tanzania aliipongeza LG kwa kutengeneza fursa kwa wananchi kupitia vifaa vyake vya kielektronic na bidhaa ambazo ni maarufu sana Tanzania*.
“Tunaipongeza LG kwa mchango wao katika uchumi wetu na tunawahakikishia kuwa serikali inaunga mkono kwa kutengeneza mazingira rafiki kwa mashirika ya ndani na ya kimataifa kufanya biashara nchini Tanzania ,” alisema Waziri Mkuu.
Kwa sasa LG inaongeza upatikanai wa huduma zake nchini Kenya, Tanzania, Ethiopia na Sudani, Kwa kufungua maduka mapya na kuboresha yale yaliyokuwepo, kwa lengo la kuweza kukidhi mahitaji yanayozidi kuongezeka ya vifaa vya nyumbani, burudani na bidhaa za nywele.
MwishoKUHUSU LG ELECTRONICS, INC.LG ni kampuni ya kimataifa ya uvumbuzi katika teknolojia na vifaa vya kielektroniki, kampuni ambayo iko katika karibu kila nchi na yenye nguvu kazi ya wafanyakazi wa kimataifa zaidi ya 75,000.
Makampuni manne ya LG – Home Appliance & Air Solution, Home Entertainment, Vehicle component Solutions na Business Solutions kwa Pamoja yametengeneza mauzo ya kufikia dola bilioni 63 ulimwenguni kote mwaka 2021.
LG ni kampuni inayoongoza katika uzalishaji wa bidhaa za walaji na kibiashara ambazo ni Pamoja na TVs, Vifaa vya nyumbani, Viyoyozi, Monitors, Roboti za Kutoa huduma, vifaa vinavyojiendesha vyenyewe na chapa yao ya kiwango cha juu na yenye utambuzi LG ThinQ ni majina yanayofahamika duniani kote.
Tembelea www.LGnewsroom.com kwa taarifa za hivi karibuni.
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi