Wanaume wanne wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Lebanon Rafik Hariri na watu wengine 21 katika shambulio la bomu mwaka 2005, wanatarajiwa leo kutolewa uamuzi kuhusu kesi hiyo inayowakabili.
Watuhumiwa wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kishia wa kundi la Hezbollah nchini Lebanon – walihukumiwa na mahakama maalum huko Uholanzi licha ya kutokuwepo mahakamani.
Hasira iliyojitokeza baada ya shambulio la Beirut ililazimu Syria iliyokuwa inaunga mkono kundi la Hezbollah kuondoa vikosi vyake Lebanon miaka 29 iliyopita.
Hezbollah na serikali ya Syria zilikanusha kuhusika na shambulio hilo.
Zaidi ya watu 220 walijeruhiwa pale gari lililokuwa limejazwa vilipuzi lilipolipuka wakati msafara wa Bwana Hariri ulipokuwa unapita mbele ya ufuo wa Beirut.
Mauaji hayo yalibadilisha Lebanon na kuanza kuchipuka kwa makundi ya upinzani ambayo miaka kadhaa baadae yalibadilisha siasa za nchi hiyo.
Kijana wa Bwana Hariri, Saad, aliongoza chama kilichokuwa kinapinga Syria na kuunga mkono nchi za Magharibi na yeye mwenyewe akahudumu kama Waziri Mkuu kwa mihula mitatu.
Anatarajiwa kuhudhuria kikao cha mahakama maalum kwa Lebanon, chenye makao yake viungani mwa The Hague, umamuzi huo unapotolewa Jumanne.
Hadi kufikia sasa hakuna taarifa zozote kuhusu walipo washukiwa hao Salim Jamil Ayyash, Hassan Habib Merhi, Hussein Hassan Oneissi and Assad Hassan Sabra
Hakuna kati yao aliyesema chochote wakati wa kesi inaendelea. Lakini mahakama iliteua wakili atakayewawakilisha aliyetupilia mbali taarifa za mwendesha mashtaka akidai kwamba ziliegemea ushahidi wa kawaida tu uliokosa uthabiti na kushindwa kuthibitisha kwamba bila shaka yoyote watuhumiwa walikuwa na makosa.
More Stories
Dk. Mpango amwakilisha Samia sherehe za Uhuru wa Lesotho
Samia atangaza Tanzania kumuunga mkono Odinga
Tanzania yaongoza kikao maalum cha nishati safi