Na Mwandishi Wetu
DAWA za Viagra ambazo wengi tunajua kuwa hutumiwa zaidi na watu ambao wamepoteza uwezo wa nguvu za kiume, inaweza kusimamisha maua yaliyokatwa kwa siku saba.
Kwa mujibu wa timu ya watafiti kutoka nchini Israeli wakishirikiana na wanasayansi wa Australia, waliyeyusha dawa hiyo na kuamua kujaribu uwezo wake katika maua yaliyokatwa na jambo la kushangaza maua hayo yalisimama na kuchangamka kwa wiki moja zaidi ya muda wake wa kuishi.
“Kipimo cha miligramu moja ya Viagra ikiyayushwa kwenye maji yaliyoko katika vyombo vyenye maua, mmea huo unaweza kukaa muda mrefu na kupunguza kasi ya kunyauka mara 5 zaidi ya uhai wake,” walisema wanasayansi hao.
Hata hivyo, ilionesha kuwa, dawa hiyo inauwezo wa kupunguza maua kunyauka kwa baadhi ya matunda kama vile strawberries, mbogamboga na maua mbalimbali
More Stories
Rungwe yajenga soko kukuza uchumi kwa wananchi
Waislamu Mwanza wapokea Ramadhani kwa maandamano ya kidini
Kamati ya kudumu ya Bunge ya utawala,katiba na sheria yaridhishwa ujenzi soko Kariakoo