Na Mwandishi Wetu
Utakapoamua kujifungia katika giza totoro unaweza kuwa kipofu. Kwa mujibu wa wachambuzi kutoka tovuti elimishi ya quora, tatizo hili linaweza kuwa ni la muda tu na hali yako kurudi baada ya muda.
Hata hivyo, ukikaa katika giza kwa siku tatu mfululizo utapofuka na kusababisha hisia zingine za mwili wako kufunguka zaidi na kukufanya uweze kufanya mambo bila kuona.
Macho ni moja ya baraka tuliyopewa, kuishi bila macho ni dhana inayotisha. Mambo mengi tunayofanya kila siku hutafsiriwa kwa kupitia macho kwenda kwenye ubongo.
Ni kweli tunategemea sana macho yetu, kama hatuoni, ni ngumu kuelewa na tutashindwa kufanya mambo mengi ya kila siku. Pata picha maisha bila macho, japo ni vigumu, lakini umeshawahi kufikiria watu wenye ulemavu wa kutoona? Watu milioni 39 duniani hawaoni.
Kila mwaka maelfu ya watoto wanazaliwa na upofu. Wengine hupofuka kutokana na magonjwa.
Tiba nyingi zinafanyiwa utafiti, japo baadhi ya magonjwa yanayosababisha upofu hayatibiki. Watafiti wengi pia wanaendelea kujitahidi kutengeneza macho ya bandia.
More Stories
SHUWASA yaboresha mtambo wa kuchakata takakinyesi
Daktari ajishindia milioni 100,fainali NMB Bonge la Mpango
Majaliwa ataka tenki la Kisesa lianze kutoa maji Februari