Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MSANII wa muziki wa Hip hop Tupac Shakur aliyepata umaarufu mkubwa duniani na kupoteza maisha kwa kupigwa risasi katika ugomvi uliohusisha kurushiana risasi mwaka 1996 nchini Marekani katika jiji la Las Vegas, alikumbukwa na kundi aliloanzisha la Outlawz kwa kuchanganya majivu ya mwili wake na bangi na kisha kuvuta kama sigara.
Katika mahojiano na televisheni ya VladTV, kundi la The Outlawz walithibitisha uzushi uliokuwa ukisambaa kuwa kundi hilo lilichanganya majivu ya Tupac na bangi kisha kuvuta “smoked him out” kama heshima yao ya mwisho.
Kwa mujibu wa gazeti la The Independent la nchini Uingereza na https://www.huffpost.com/entry/outlawz-confirm-they-smoked-tupacs-ashes_n_942106, mmoja wa wasanii wa kundi hilo, Noble, alithibitisha kwa kusema, “Ndio ni kweli kabisa…tulikuwa katika kumbukumbu na familia yake pamoja na mama yake .
Tukio hilo lilitokea katika kumbukumbu ya miaka 15 tokea kifo cha Tupac kilichotokea tarehe 13, Septemba 1996 ambapo marafiki na mashabiki wake walikutana katika kumbukumbu hiyo.
Kwa mujibu wa mtandao wa BET, marafiki zake wa muda mrefu wa Tupac Shakur, The Outlawz, wamedai kumkumbuka rafiki yao ambaye pia ndio mwanzilishi wa kundi hilo kwa namna ya pekee.
Mtaalam wa masuala ya mifumo ya upumuaji, Dkt.Clifford Bassett kutoka jijini New York, Marekani akizungumzia juu ya hatua hiyo anasema,mtindo wa maisha ya kuiga na kuvuta vitu ambavyo havijaidhinishwa na wataalam wa afya ni hatari zaidi.
More Stories
Lishe bora suluhisho la udumavu ,utapiamlo
KWA TAARUFA YAKO :Masabuni alinusurika kifo katika Meli ya Titanic
KWA TAARIFA YAKO: Ajifungia kichwa ili kuacha kuvuta sigara