TAARIFA ya Hali ya Uchumi wa mwaka 2023 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa 2024/2025 iliyowasilishwa na Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, imeainisha mafanikio mengi ambayo yamepatikana katika kipindi cha miaka mitatu cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Kutokana na mafanikio hayo, Prof. Mkumbo anatoa oongezi za dhati kwa Dkt Samia, kwa jinsi anavyoliongoza Taifa letu kwa weledi, umahiri na utulivu mkubwa.
Katika kipindi chake cha miaka mitatu, Dkt Samia ameonesha weledi na kuthibitisha ubunifu na uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yake.
Zaidi ya yote, Rais Samia amethibitisha kuwa kiongozi muungwana na mpenda haki, kupitia falsafa yake ya uongozi ya 4R, amejenga maridhiano mapana ya kijamii na kisiasa, na kuweka mazingira sawia ya kufanya siasa kwa vyama vyote nchini.
Ametoa uhuru wa kutosha wa kutoa maoni bila woga wala vitisho huku akionesha utulivu wa hali ya juu.
Kiongozi wetu aliyeleta mageuzi makubwa katika kuweka mazingira bora ya uwekezaji na kufanya biashara.
Ameimarisha sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na kuwapa matumaini mapya wakulima na wafugaji na wachimbaji wadogo wa madini.
Lakini pia Rais Samia amekuwa na maono yanayolenga kuifungua nchi katika sekta mbalimbali.
Mfano siku zote, Rais Samia anasisitiza kuboreshwa kwa diplomasia ya kiuchumi na hili limewezesha kuifungua nchi katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na mazungumzo na ugeni wa namna hii
Pia Rais Samia amekuwa akibainisha maeneo kadhaa ya kimkakati yanayoiwezesha Tanzania kuwa kivutio cha uwekezaji ambayo ni pamoja na utulivu wa kisiasa, fursa na vivutio anuai vya uwekezaji, mifumo thabiti ya kisheria, vigezo vya kijiografia vinavyoifanya Tanzania kuwa kiunganishi na nchi nyingine za mashariki, magaharibi na Kusini mwa Afrika, ukarimu wa Watanzania pamoja na maliasili zilizopo.
Hakika anaijenga upya nchi yetu na kupitia uongozi wake serikali na nchi yetu ipo salama.
More Stories
Tanzania Yaibuka Kidedea: Uongozi wa Rais Samia waboresha weledi wa Jeshi la Polisi
Tuhimize amani kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Ana ahidi,ana tekeleza,maneno kidogo,vitendo vingi