July 14, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kutofahamika kwa taasisi za uwezeshaji kiuchumi nchini chanzo Cha umasikini

Na Israel Mwaisaka,Nkasi

‎KUTOKUWEPO kwa taarifa sahihi juu ya Taasisi zinazoweza kuwasaidia Wananchi katika kujikwamua kiuchumi ni mojawapo ya visababishi vinavyopelekea jamii kuendelea na umasikini .

‎Hayo yamesemwa na Mbunge wa viti maalumu mkoa Rukwa na ambaye pia ni mratibu wa mafunzo ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi Jacguline Mzindakaya   kwenye ufunguzi wa mafunzo kwa jamii ya utoaji wa elimu kuhusu Fursa za mitaji kupitia mifuko na programu za uwezeshaji Wananchi kiuchumi mkoani Rukwa.

‎Alisema kuwa hapa nchini Kuna taasisi nyingi ambazo zimelenga kuwasaidia wajasiliamali kuweza kukua kiuchumi na kuwa kama taasisi hizo zikifahamika vyema  basi Wananchi watazitumia na kuweza kuyafikia malengo Yao makubwa katika kupambana na adui umasikini.



‎Mzindakaya alidai kuwa mkoa Rukwa ni moja kati ya mikoa iliyobarikiwa kuwa na fursa nyingi na ardhi yenye rutuba na kama taasisi hizo za uwezeshaji kiuchumi Wananchi zikifahamika vyema Wananchi watazitumia na kuweza kuufikia uchumi unaotakiwa.

‎”tunayo mashirika na taasisi mbalimbali za uwezeshaji Wananchi kiuchumi lakini hazijulikani hivyo katika mafunzo haya Kila mmoja awe makini katika kuzitambua taasisi hizo ikiwa ni pamoja na namna ya kuweza kuzikia”alisema Mzindakaya



‎Alidai kuwa kulingana na fursa zilizopo mkoa Rukwa na Wananchi wake kuendelea kuwa masikini lakini kisababishi kikuu ni taasisi hizo za uwezeshaji jamii kiuchumi kutotambulika sawa sawa na Wananchi kushindwa kuzitumia.

‎Kaimu Katibu mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji kiuchumi (NEEC) Gwakisa Bapaya aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha wanayaelewa na kuwa mabalozi kwa wengine katika kuzifikia fursa kupitia mashirika na taasisi za uwezeshaji kiuchumi.

‎Alidai kuwa taasisi za uwezeshaji kiuchumi zimewekwa na Serikali kama vyombo vya kuchagiza maendeleo kwa jamii hivyo wanayo fursa ya kuzitumia taasisi hizo kwani zimeundwa kwa ajili Yao na kubwa ni kuwasaidia Wananchi hasa wajasiliamali kuweza kujikwamua kiuchumi.

‎Mkuu wa Wilaya Nkasi Peter lijualikali kwa upande wake aliwasihi washiriki wa mafunzo hayo pale watakapomaliza kuwafanya kwa vitendo kwa kuhakikisha taasisi hizo za uwezeshaji kiuchumi zinafikiwa kwa wingi na kuwa hiyo ndiyo njia pekee tutayoweza kuondokana na lindi la umasikini.

‎Mashirika na taasisi za uzesheshaji chini ya Baraza la Taifa la uwezeshaji kiuchumi (NEEC) yaliyoshiriki katika utoaji wa mafunzo hayo ni TaFF,SELF MF,CRDB,TADB,SIDO,AGTIF,AZANIA BANK,BOT,NMB,EFTA,PASS Leasing,YDF,COSTECH na nyinginezo