Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Dar
MEYA wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto ambaye ni Diwani wa kata ya Vingunguti wilayani Ilala amepongeza idara ya mazingira kwa kudumisha usafi amewataka wana Ilala kudumisha usafi ili tuendelee kuwa kinara wa usafi
Kumbilamoto amesema hayo kata ya Kivukoni katika kampeni ya usafi wa Mwisho wa Mwezi ambapo aliwataka wananchi wa Ilala kudumisha usafi kwa kushirikiana na idara ya mazingira ili tuwe kinara wa usafi Dar es Salaam.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Balozi wa Mazingira Duniani nchi yetu sasa hivi wananchi wanatumia nishati safi bila kuchafua mazingira hivyo ni jukumu kubwa katika kumuunga mkono Rais Dkt.Samia,”amesema.
Kumbilamoto ameipongeza idara ya mazingira Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kudumisha usafi na kutengeza bustani za Halmashauri hiyo.
Afisa Mazingira Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Theresia Mwakasungura,amesema kuwa dhumuni la kufanya usafi huo ni kuhamasisha jamii katika suala zima la usafi kwani usafi ni mkakati wa Kitaifa.






More Stories
CCM kusimamia kitabu cha Hayati Songambele kiingie mtaani
Mwendokasi kuendeshwa na ENG kwa miaka 12
Vitongoji 284 Arumeru Mashariki vyafikiwa na umeme