Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Dar
MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Vingunguti wilayani Ilala mkoa Dar-es-Salaam kupitia Chama Cha Mapindizi (CCM),Omary Kumbilamoto, amesema serikali chini ya chama hicho imefanya mambo makubwa katika mtaa wa Majengo ikiwemo miundombinu ya barabara ya kisasa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Vingunguti mtaa wa Majengo,Kumbilamoto, miundombinu hiyo ni pamoja na mtandao wa barabara za kisasa Vingunguti ikiwemo kilima chaka chui pamoja na kalavati.

Pia katika kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025, Serikali ilitoa fedha za kujenga barabara kiwango cha lami pamoja taa za nishati ya jua(solar), Vingunguti mpaka Mnyamani kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kiasia cha milioni 304,huku mtandao mwingine wa barabara ulijengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Km 1.9, unaounganisha mtaa huo na mtaa wa Kombo.
“Mafanikio mengine ni sekta ya uchumi ndani ya Kata ya Vingunguti Mtaa Majengo ni pamoja na mradi wa soko la nyama choma ambalo linatoa huduma ya interneti bure na linapokea wageni kutoka ndani na njema ya nchi.Pia kwa sasa Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam inakusanya zaidi ya milioni 12 kupitia soko hilo,”amesema .
Sanjari na hayo amesema jeshi la polisi limefanikiwa kuimarisha suala la ulinzi na usalama katika Kata ya Vingunguti na kuchochea biashara kufanyika muda wote huku vitendo kwa kihalifu vikiwa vimepingua.
Hivyo amewaomba wananchi wa Kata hiyo kuwapigia kura wagombea wa nafasi mbalimbali ikiwemo Uraisa, Wabunge na Madiwani wanaotokana na CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako