Na Bakari Lulela, Timesmajira Online,Dar
Mgombea wa nafasi uenyekiti wa Serikali za Mitaa kwa tiketi ya Chama Cha Mapindizi (CCM) katika eneo la Mkunduge Kata ya Tandale jijini Dar es salaam Said Mrisho,ameahidi kuboresha miundombinu sambamba na kujenga ofisi ya kisiasa mara atakapo pata ridhaa ya kuchaguliwa kwa nafasi hiyo.
Hayo ameyabanishwa Novemba 23,2024,katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Rasco jijini Dar-es-Salam.
“Naomba ridhaa ya kunichagua mimi pamoja na wajumbe wangu katika kusimamia Ilani ya CCM, ambapo ahadi yangu ya kwanza ni kujenga ofisi ya kisasa sambamba na kuboresha miundombinu ikiwemo barabara na ujenzi wa kingo katika mto Mwandosi uliopo kwenye eneo hili,” amesema Saidi.
Kupitia ilani ya CCM,atahakikisha anashirikiana na wajumbe wake kufanya kazi za chama kwa kuwahudumia wananchi wa Mkunduge,na kusimamia vema suala la ulinzi na usalama wa mtaa kwa kushirikiana na wananchi wake.
Aidha amesema, kuwa kutokana na hali kuwa ngumu ya wanawake wengi kuchukua mikopo umiza,atakapopata ridhaa atahakikisha anamaliza matatizo mbalimbali yanayohusu mikopo pamoja na kuwapatia fursa vijana ili waweze kujiajiri au kuajiriwa sehemu mbalimbali.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani amejizatiti kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini ikiwemo kutengeneza reli ya kisasa (SGR) na kujenga miundo mbinu saidizi kote nchi mzima hivyo wachagueni viongozi hawa ili waweze kumsaidia mama katika kuwatumikia watanzania.
.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu