January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kuelekea Tigo Kili Half Marathon wananchi wajitokeza Dar

WANANCHI wa Riadha wamejitokeza katika viunga vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Kuchukua namba na Vifaa vya kukimbilia kuelekea Mbio za Kimataifa za Tigo Kili Half Marathon 21Km ambazo zimedhaminiwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo, zitakazofanyika Jumapili ya Februari 25, 2024 Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.

Hadi sasa, nafasi kwa ajili ya kukimbia Mbio hizi Maarufu za 21Km tayari zimejaa ( SOLD OUT ) na zoezi la Kugawa Namba linaendelea Leo Februari 17 – 18 Kwa upande wa Dar Es Salaam , Arusha Februari 20 – 21 Kisha Moshi Februari 22 – 24.

Suzana Mathias, Khamis Salehe na Kassim Swedi ni Miongoni mwa watakaoshiriki mbio hizi Februari 25, wakizungumza na Mwandishi wetu kwa nyakati tofauti tofauti wameipongeza Kampuni ya Tigo kwa kuendelea kudhamini mbio hizi kwa miaka kadhaa mfululizo.

Kwa upande wake Suzana amesema yeye hajawahi kushiriki Half Marathon amekua akishiriki mbio nyingine za Km 5, ila safari hii kaamua kushiriki Half Marathon Km 21, kutokana na mchango wa Tigo katika jamii hasa kupitia Promosheni zao mbalimbali.