Na Rose Itono,TimesMajira Online
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya Chama cha ACT-Wazelendo, Saed Kubenea amewataka wananchi wa jimbo hilo wamchague ili aweze kusimamia maendeleo na maslahi ya wanyonge.
Akizungumza wakati akizindua kampeni zake kwenye viwanja vya Buibui vilivyopo Mwananyamala juzi, Kubenea amesema Jimbo la Kinondoni lina changamoto nyingi ambazo haziwezi kutatuliwa na Mbunge wa chama kingine zaidi ya ACT-Walendo.
Amesema endapo atachaguliwa kwenye uchaguzi unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu, atahakikisha anasimamia maendeleo na maslahi ya wanyonge kwa kuhakikisha wanapata maisha ya raha.
“Mbali na kusimamia maendeleo na maslahi ya wanyonge, pia nitaondoa kero ya mafuriko kwa wananchi wa jimbo langu kwa kuufukia Mto Msimbazi na kubadilisha eneo hilo kuwa kivutio cha utalii,” amesema Kubenea na kuwaomba kura wananchi wamchague ili awe mbunge wao.
Amesema ataboresha matumizi ya fedha za mfuko wa mbunge kwa kuhakikisha unawaletea maendeleo wananchi kwa kuwapatia mikopo.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu