TAFITI moja kutoka nchini Australia imeonesha ya kuwa kwa kila saa mtu anavyoketi kuangalia luninga hupunguza uhai wake kwa dakika 22 .
Kuketi kwa saa moja mfululizo huathiri uwezo wa mwili wa kudhibiti sukari,shikizo la damu na kutumia mafuta hivyo huongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo,kisukari na saratani.
Vilevile kukaa kwa muda mrefu huongeza uwezekano wa mwili kutonyooka vizuri na kusababibisha maumivu wa mgongo uzeeni taarifa hii ni kwa mujibu wa kitabu cha Mtindo wa maisha na magonjwa yasiyoambukiza.
Inashauriwa kufanya mazoezi ya mwili mfano simama,tembea,nyoosha viungo na kadhalika kwa dakika moja hadi mbili kila baada ya saa moja ya kuketi .
Jaribu kupunguza muda wa kuangalia mfululizo wa luninga na kompyuta na badala yake ongeza muda wa kufanya mazoezi .
Simama wima badala ya kuketi hii hupunguza uwezekano wa kupata maumivu ya mgongo na kukunjika uzeeni.
More Stories
Furaha ya kila mwanamke ni kuwa mama
Ijue nyota yako ili kufanikiwa kimaisha, mahusiano na ndoa
Ijue mbinu sahihi ya kuwakabili wezi