Na Joyce Kasiki,Timesmajira online
MKUU wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dkt.Joyce Nyoni amesema,chuo hicho kimeanza udahili wa kozi mpya ya malezi na makuzi ya mtoto ili kupata wataalam watakaoenda kutoa elimu hiyo kwa jamii na hivyo kuleta malezi chanya kwa watoto.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara kwenye banda la Taasisi ya Ustawi wa Jamii,Dkt.Nyoni amesema,kozi hiyo ni muhimu hasa katika nyakati hizi ambapo kumekuwa na matukio mengi ya ukatili.
“Kama mnavyojua,kumekuwa na matukio mengi ya ukatili hasa kwa watoto,hii ni kutokana na jamii kutokuwa na uelewa wa malezi na makuzi ya watoto na namna wanavyoweza kuathirika na malezi yasiyofaa.”amesema Dkt.Nyoni
Kwa mujibu wa dkt.Nyoni , mtaala huo mpya unakwenda kuwasuka wakufunzi na wataalamu wa malezi,makuzi na mawndeleo ya awali ya mtoto kwa ajili ya kwenda kufundisha walimu wanaofundisha watoto, walezi wa watoto pamoja na wale wa kwenye vituo vya kulelea watoto wadogo.
“Kozi hii mpya itatolewa kwa ngazi ya Cheti na Diploma katika Kampasi yetu ya Kisangara Mwanga Mkoani Kilimanjaro na tumaamini katika miaka ijayo inakwenda kuleta tija kwenye malezi ya watoto hapa nchini.”amesisitiza
Amesema tayari Chuo kimeshanza kudahili wanafunzi huku akiwaasa Watanzania hususan vijana wenye sifa kuomba kozi hiyo
“Jamii inakabiliwa na changamoto ya malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ,wengi hawajui faida za malezi chanya hasa katika miaka ya awali ya mtoto kwa hiyo hawa wataalam wanakwenda kufundishwa namna ya kumsaidia mtoto katika nyanja muhimu ili wakue vyema”amesisitiza
mroro amefafanua kozi hiyo itakwenda kutoa suluhisho kusaidia kuweza kuwajenga kuhusiana na malezi ya watoto kwani jamii inakabiliwa na changamoto kubwa katika malezi hayo ikiwemo kuwepo kwa ukatili kwa watoto.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria