Na Daud Magesa , Timesmajira Online, Mwanza
Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza,wamemchagua Bhiku Kotecha ,Diwani wa Kata ya Nyamagana kuwa Naibu Meya kwa kipindi kingine cha mwaka mmoja.Uchaguzi huo umefanyika Septemba 10,2024,baada ya kumaliza muda wa awali,na kupendekezwa tena na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi hiyo.
Uchaguzi huo umefanyika kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Halmashauri ya Jiji la Mwanza za mwaka 2013, kanuni namba 7 (3).
Katika uchaguzi huo,Kotecha alipata kura 21 kati ya 22 zilizopigwa, huku kura moja ikiharibika.Ofisa Uchaguzi Jiji la Mwanza, Lilian alimtangaza Kotecha kuwa Naibu Meya kwa kipindi hiki kipya cha 2024/2025.
Akizungumza baada ya kutangazwa Kotecha,aliwashukuru Madiwani hao,kwa kumchagua tena,huku akiahidi ushirikiano kwa ustawi Halmashauri na wananchi wa Jiji hilo.
Kwa upande wake,Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Deogratius Nakey,amewataka,Madiwani kuwa wamoja na waanze upya kuwahudumia wananchi.Huku akisisitiza wakawawajibishe wataalamu wanaokiuka viapo.
More Stories
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais