Na Allan Vicent, Igunga
JESHI la Polisi wilayani Igunga Mkoani Tabora limemkamata Kitundu Godfrey (35) mkazi wa Mtaa wa Stoo, Kata ya Igunga na kumfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wilayani humo kwa tuhuma za kumfanyia ukatili wa kingono mtoto wa miaka 4.
Mwendesha Mashitaka wa Polisi wilayani humo Elimajid Kweyamba alisema mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu 138 C (1) (2)(b) kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2019 inayozuia kutenda makosa kama hayo.
Aliiambia mahakama mbele ya hakimu wa wilaya Eddah Kahindi kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kati ya Juni 1, na Agosti 31, mwaka muda wa mchana na usiku katika mtaa huo.
Alisema mshitakiwa akiwa na mihemko ya kingono alimfanyia ukatili mtoto huyo kwa kumwingizia vidole sehemu zake za siri na kumsababishia maumivu makali mwilini mwake.
Hata hivyo baada ya kusomewa shitaka mtuhumiwa amekana kutenda kosa hilo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 16, mwaka huu itakaposikilizwa tena,mshitakiwa amepelekwa mahabusu.
More Stories
RC Mrindoko:Ufyekaji wa mahindi Tanganyika si maelekezo ya serikali
Walimu S/ Sekondari Ilala wafundwa juu ya maadili ya wanafunzi
Dkt. Samia afungua skuli ya sekondari Misufini, Bumbwini